IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000
JUMLA
ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya
programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika
ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Pia
maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki
zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na
kujifunza kwa gharama nafuu.
“Lengo
la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu
ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo
itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa
‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,”
alisema Profesa Bhalalusesa.
Kamishina
wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella
Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya
Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea
katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Katika
maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia
wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea
yataimarisha kiwango cha elimu.
“Dunia
imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi
kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu
ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
Alisema
wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza
kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na
hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa
wanafunzi.
Profesa
Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali
waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia
mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na
watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi
ya sekondari.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.