Wednesday, 23 September 2015

Shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 1.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma akiwa katika moja ya madawati yaliyotolewa.


 Walimu wa shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurungezi wa manisipa ya Kinondoni pamoja na maaofisa wa Aggrey&Cliffor

 Wanafunzi wanao soma shule ya awali katika shule ya msingi mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa manisipaa ya kinondoni na maaofisa wa Aggrey&Clifford

No comments:

Post a Comment