Thursday, 23 June 2016

BUSINESS ADMINISTRATORS ASSOCIATION FROM TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) THEY BRING TO YOU BBA LAUNCHING AND ENTERPRENEURIAL SEMINAR


BAA launching and entrepreneurial seminar which will be held at Tanzania Institute of Accountancy on this  Saturday at 10 am up to 2pm.
The main speaker Maida Waziri, President of voice of Women Entrepreneurs Tanzania and Managing Director of IBRA Contractors Ltd.






A retired president of Business Association Mr.Elisha Bernad (at the center) and his cabinet in a group phtoto .


They are showing a flies which show the description of the event which will be held at their institute on this Saturday.



All student at TIA  and near colleges your mostly invited at this event so as you can gain more experience and exposure.




 
 TIASO President (at the middle with jeans trouser) showing a support to the BAA Association on advertising their event.

For more story about this

  Umoja mpya wa wanafunzi wanaosoma uongozi wa biashara katika chuo cha Uhasibu Tanzania(BAA-TIA),wakishirikiana na kamati wezeshi wanatarajia kufanya semina ya ujasiriamali siku ya jumamosi ya tarehe 25 mwezi wa sita mwaka 2016 sambamba na kutambulisha rasmi umoja huo kwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho.
Semina na uzinduzi huu umekuja kama neema kwa wanafunzi wa vyuo vya juu hasa kwa  wanaomalizia masomo yao kwa mwaka wa tatu wa shahada,mwaka wa pili wa stashahada na wale wanaochukua astashahada katika chuo hiki cha uhasibu.
Umoja huu uliondwa kwa lengo la kuhamasisha elimu ya kujituma na uelewa halisi wa maswala ya biashara pamoja na kumpa uzoefu mwanafunzi husika katika fani ya uongozi wa biashara unategemewa kuleta matunda bora katika tasnia ya uongozi pamoja na kuimarisha mahusiano na taasisi zinginezo zinazofundisha masomo ya biashara.
Mgeni mzungumzaji mkuu katika semina hii anatarajiwa kuwa mama Maida Waziri mkurugenzi wa kampuni ya IBRA Contractors.
Hii imewezekana kufuatia ushirikiano wa wanafunzi pamoja na wakufunzi wanaofundisha masomo ya ujasiriamali shuleni hapo wakiongozwa na mkufunzi mama  A.Lauwo,Mwenyekiti mwezeshaji Ndugu Gwamaka Andrew,Alex Mujwahuzi kama Katibu Mwezeshaji, kiongozi wa darasa Lidya Ndomba ,Theresia Chacky,Richard Mwakatumba,Imelda Mitti pamoja na Irene Mbura
 Kuhusu Umoja wa wanafunzi wa Masomo ya biashara
Umoja huu ni umoja mpya kabisa kwa chuoni hapo ambapo kabla ya kupata viongozi wa kutoka madarani ulikua chini ya kamati ya darasa la wanafunzi wa mwaka wa tatu.
Wanafunzi hawa wanaokaribia kumaliza mwaka wao wa masomo walianza jitihada zao hizi za kuanzisha umoja huu wakiwa mwaka wa pili ambapo kamati iliundwa na wanadarasa kukamilisha zoezi kamili.
Kamati hii ilikua na mwenyekiti ndugu Elisha Benard, msaidizi wa mwenyekiti Maryam Seif, katibu Peter Charles ,msaidizi wake Irene Mbura na Muhidini Mdanku kuwa mweka hazina.
Pamoja na hao kamati ilichagua wapangaji matukio ndugu Alex Mujwahuzi na bi Grace Semagoda, viongozi wa darasa Bi.Consolata Mayokolo na Bw. Albert Washenta walichaguliwa kuwa wahamasishaji wakuu kwa nafasi zao kama wawakilishi wa darasa.
Ndugu Jeremiah Ngalla alichaguliwa kuwa mkuu wa kitengo cha Tekinolojia Mawasiliano akiungana na Gabriel Lucas,Jimmy Wilbert,Yusuph Kaseko,Yusuph Idd na Othmani Panyika.
Wajumbe wengine Katika kamati hii ni Jaquiline Mwayole,Godfrey Balyo,Samweli Ngwavi,Diana Muganyizi,Emanuel Chagoha,Maimuna Anjechele,Martin Bayona ,Shabani Jumapili,Josephine Joseph na Michael Ngosha.
Kamati hii waanzilishi waliweza kuandaa katiba iliyopitiwa na mwanasheria wa chuo Bw.Mayunga na kuruhusiwa kuendelea na zoezi la kupata uhalali kutoka ngazi nyingine za chuo.
Kamati iliwakilisha barua ya maombi kwa Mkuu wa Idara ya Masomo ya uongozi wa biashara na Masoko Bw.Lucas Ng’webeya ambaye alipenda kazi iliyofanya na kamati hii na kuahidi ushirikiano kutoka kwake.
Barua rasmi ya kuomba kutambuliwa na uongozi iliandikwa kwenda kwa mkuu wa chuo na kukubaliwa kuendelea na zoezi la kuutangaza umoja na kufanya zoezi la uchaguzi.
Tarehe 22 mwezi wa Sita , Umoja huu ulifanya uchaguzi wake wa Awali na kupata viongozi wake Mwenyekiti William Msemo,msaidizi wake Seleman W. Selemani, katibu wa umoja Singizi Hassani na msaidizi wake Shokolo Kashindye.
Bi Halima Salehe Machalina alichaguliwa kuwa mweka hazina wa Umoja huu,uchaguzi huu ulienda sambamba na kuchagua wawakilishi wa madarasa waliongia katika vitengo vya Tekinolojia Habari , Mawasiliano na uenezi, itifaki na katiba pamoja na kitengo cha mipango.
Walioingia kwenye kamati ya Tekinolojia Habari ni ndugu Daniel O.Lyamula, Ramadhani Mohamedi na Rogers Alex.
Edward Albert, Hafsa Abdi Mjaka ,Scholastica Mdee ,Omari Sufiani na Winton Elia waliingia kitengo cha habari na uenezi wakati ndugu Selemani W.Selemani ,Hassani Singizi,Samweli Elias na Kafumu John wakiingia kitengo cha katiba.
Athanasio William,Ally J Juma, Fatma Shabani na Joyce Zephania walifanikiwa kuchaguliwa na wajumbe kutoka madarasani kwao katika kamati ya mipango ya Umoja huu.
Kamati ya uwezeshaji na kamati Anzilishi ya umoja wa wanafunzi wa masomo ya biashara unawakaribisha wote katika tukio hili jema.



No comments:

Post a Comment