Na Asnani Chionda, Morogoro.
Ikiwa inakaribia Miezi mitatu Tangia sakata la Kufungiwa kwa Chuo kikuu cha Mtakatifu joseph, tawi la songea, kutokana na chuo hicho kutokidhi vigezo vinavyohitajika kutoa elimu ya chuo kikuu, Bodi ya Mikopo imeonekana kuwasahau baadhi ya wanafunzi wanufaika wa mikopo waliohamishwa kutoka chuo hicho kwenda chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA.
Wakizungumza na SCHOLARRS BLOG, wanafunzi wa mwaka wa tatu, wapatao 120 walioripoti chuoni hapo tarehe 18/03 Mwaka huu ambao wamepangiwa kusoma shahada ya Sayansi na teknologia ya chakula (kutoka Shahada ya uhandisi wa uandaaji na uzalishaji wa chakula waliokuwa wanasoma St Joseph) na wale wa shahada ya teknologia ya kilimo(BTAG) chuoni hapo, wanaelezea adha ya ugumu wa maisha wanayoishi kutokana na bodi ya mikopo kutowapelekea pesa za kijikimu kwa kipindi cha miezi mitatu tokea wahamishiwe chuoni hapo.
Mmoja wa wanafunzi hao ( Jina tumelihifadhi) akuzungumza kwa maskitiko makubwa alisema "Tupo hapa zaidi ya miezi miwili sasa, tumevumilia vya kutosha, tumepewa ahadi nyingi na viongozi wa bodi na Tume ya vyuo vikuu juu ya pesa zetu, lakini had leo, hakuna dalili za kupata pesa hizo" pia mwanafunzi huyo aliongeza kuwa, licha ya wanafunzi hao zaidi ya 120 majina yao kuonekana kwenye listi ya wanafunzi wanaostahili kupata pesa hizo, lakini mpaka sasa bodi ya mikopo haioneshi dalili ya kutoa pesa hizo, hivyo wanafunzi hao wanapenda tutoa wito kwa bodi ya mikopo kuharakishwa kutolewa kwa pesa hizo kwani hali inazidi kuwa mbaya na kuharibu hali na uwezo wa kusoma kwa wanafunzi hao wakiwa chuoni hapo.
Aidha wanafunzi hao wanapenda kutoa rai kwa wazazi wao juu ya hali zao kimaisha kwani wapo baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao hawaoneshi ushirikiano kwa watoto wao juu ya pesa za kujikumu kwa kudhania kuwa watoto wao wamepokea pesa kutoka bodi lakini wanawadanganya wazazi wao, kitu ambacho si cha kweli na kinasababisha wanafunzi hao kuishi maisha magumu zaidi kwa kukosa sapoti ya kifedha kutoka kwa wazazi wao.
It's painful!
ReplyDeleteWorry out hope soon every thing will be okay
DeleteYaan sijui wanawaza nini hawa watendaji wa bodi ya mikopo..
ReplyDeleteKuweni na subria na imani habari imewafikia na watawashukulikia hivi karibuni na poleni sana
DeleteNi jambo la kukosa utu kwani wanatambua ni kwa jinsi gani pesa hizo zilivyo muhimu kwa wanafunzi
ReplyDeletePole sana ndugu!tuzibi kuwakumbusha naa imani wameshaupata ujumbe.
Delete