Thursday, 24 September 2015

ST.JOSEPH & FORODHANI ALUMINI

ST.JOSEPH & FORODHANI ALUMINI KUFANYIKA JUMAMOSI HII SEPTEMBA 26,2015 VIWANJA VYA ST.JOSEPH CATHEDRAL HIGH SCHOOL JIJINI DAR ES SALAAM.

Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya Joseph convent school ya jijini Dar es salaam iliyodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969,Na Forodhani Secondary iliyokuwepo kati ya 1970  hadi 2008 (ilipotaifishwa na serikali) na baada ya hapo kuwa St,Joseph Cathedral High School 2009 (baada ya kurudishwa kwa kanisa Katoliki) hadi leo,tumeungana na kuitwa St.Joseph &Forodhani ALUMIN.

St.Joseph & Forodhani ALUMIN imeanda "reunion" mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi tarehe 26 September kwa wanafunzi wote waliosoma shule hizo tajwa hapo juu bila kujali umri,jinsi au kabila.

Habari njema kuna wanafunzi waliosoma shule hii maarufu, wanaisho nje ya nchi, wanatoka Canada, Australia, New Zealand, Uingereza na Seychelles watahudhuria mkutano huu wa kihistoria.Kuna wengingine hawajafika Tanania kwa miaka zaidi ya 30,watarudi kuona shule iliowalea.

Jumamosi tarehe 26 Septemba 2015 kuanzia saa 3 asubuhi kwa shughuli mbali mbali hazi saa 7 mchana katika viwanja vya St.Joseph Cathedral High School.

Katika watu maarufu wataotoka nchi za nje atakuwepo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa ya Seychelles ambae alisoma hapa na kumaliza kidato cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo kuhamina Seychelles na wazazi wake walipo kuendelea na masomo ya juu.

Sr.Theodora Faustine
 Mkuu wa shule

No comments:

Post a Comment