Saturday, 25 June 2016

BODI YA MIKOPO YAWASAHAU WANAFUNZI WA ST JOSEPH WALOHAMISHIWA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA

Na Asnani Chionda, Morogoro. 

Ikiwa inakaribia Miezi mitatu Tangia sakata la Kufungiwa kwa Chuo kikuu cha Mtakatifu joseph, tawi la songea,  kutokana na chuo hicho kutokidhi vigezo vinavyohitajika kutoa elimu ya chuo kikuu, Bodi ya Mikopo imeonekana kuwasahau baadhi ya wanafunzi wanufaika wa mikopo waliohamishwa kutoka chuo hicho kwenda chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo,  SUA. 

Wakizungumza na SCHOLARRS BLOG, wanafunzi wa mwaka wa tatu, wapatao 120 walioripoti chuoni hapo tarehe 18/03 Mwaka huu ambao wamepangiwa kusoma shahada ya Sayansi na teknologia ya chakula (kutoka Shahada ya uhandisi wa uandaaji na uzalishaji wa chakula waliokuwa wanasoma St Joseph) na wale wa shahada ya teknologia ya kilimo(BTAG) chuoni hapo, wanaelezea adha ya ugumu wa maisha wanayoishi kutokana na bodi ya mikopo kutowapelekea pesa za kijikimu kwa kipindi cha miezi mitatu tokea wahamishiwe chuoni hapo. 

Mmoja wa wanafunzi hao ( Jina tumelihifadhi) akuzungumza kwa maskitiko makubwa alisema "Tupo hapa zaidi ya miezi miwili sasa, tumevumilia vya kutosha, tumepewa ahadi nyingi na viongozi wa bodi na Tume ya vyuo vikuu juu ya pesa zetu, lakini had leo, hakuna dalili za kupata pesa hizo" pia mwanafunzi huyo aliongeza kuwa, licha ya wanafunzi hao zaidi ya 120 majina yao kuonekana kwenye listi ya wanafunzi wanaostahili kupata pesa hizo, lakini mpaka sasa bodi ya mikopo haioneshi dalili ya kutoa pesa hizo, hivyo wanafunzi hao wanapenda tutoa wito kwa bodi ya mikopo kuharakishwa kutolewa kwa pesa hizo kwani hali inazidi kuwa mbaya na kuharibu hali na uwezo wa kusoma kwa wanafunzi hao wakiwa chuoni hapo.

Aidha wanafunzi hao wanapenda kutoa rai kwa wazazi wao juu ya hali zao kimaisha kwani wapo baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao hawaoneshi ushirikiano kwa watoto wao juu ya pesa za kujikumu kwa kudhania kuwa watoto wao wamepokea pesa kutoka bodi lakini wanawadanganya wazazi wao, kitu ambacho si cha kweli na kinasababisha wanafunzi hao kuishi maisha magumu zaidi kwa kukosa sapoti ya kifedha kutoka kwa wazazi wao.

TRA WAZINDUA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KODI KATIKA CHUO CHA IFM JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watembelea chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuzindua Jumuiya ya wanafunzi wa kodi Vyuoni katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza  na wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema kuwa jumuiya hiyo ni kwaajili ya kukuza ufahamu wa maswala mbalimbali ya kodi kwa wanajumuiya katika chuo cha IFM pamoja na wasio nanajumuiya.
amesema kupita wanachama wa jumuiya ya wanachuo hicho wawe ni chachu ya kuongeza ari wa jamii kupenda kulipa kodi kwa hiari na ni njia pekee ya kuwafikia wananchi wengi na kuibuliwa kwa vyano mbalimbali vya kodi.
Kayombo amewaasa wanafunzi wa jumuiya ya kodi vyuoni kuwa mawakala wazuri pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali katika maduka kwa kudai lisiti au kuwakumbusha wauzaji kutoa lisiti kwa wateja wao, na wateja wahakikishe lisiti iliyotolewa kama ni ya tarehe husika.

 
Makamu wa jumuiya wa wanafunzi wa Kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Amos Ojode akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.




 
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakiwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) jijin Dar es Salaam leo.


 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakiwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo chao jijini Dar es Salaam leo.



Rais wa  chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Elius Mbogo akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo
cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.


Makauma wa Rais wa chuo Usimamizi wa Fedha (IFM) akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa TRA kwa kuzindua Jumuiya ya wanafunzi wa kodi jijini Dar es Salaam leo.


Meneja Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana masala akizungumza na wanafuzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi vyuoni.

KUWA WAKWANZA TAZAMA SHULE WALIOPANGIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO JUNI 2015 KUPITIA BLOG YAKO PENDWA

BONYEZA HAPA KUTAZAMA http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/

HESLB successfully completes UoI loan beneficiary’s verification

By sadam Msunza
The process for physical verification to the loan beneficiary students at University of Iringa(UoI) held on last Friday by Higher Education Students Loan Board (HESLB) officials completed effectively without challenges to the University

Speaking to the scholar blog the public relation officer at University of Iringa Mr Crispine Nyomoye said that they facilitated HESLB officials effectively and provided everything they needed and completed their activities successfully.

He explained that the process aimed to identify students who receives loan faultily country wide , including those who receive loan more than their years of study who are not qualified to receive loan, who receive loan after leaving universities for disqualification or accomplishing their studies as well as ghost loan beneficiaries.

“The process is held countrywide and aims to find out students receiving loan five years while learning for three years also there are students who are not qualified to get loan as well as those ghost student who are not at universities and their names appear to the HESLB system” said Mr. Nyomoye

He added that inspite of the immediate announcement to students on submission of their certificates, all loan beneficiaries morw than 960 students succeded to submit their copies of certificates in appropriates time and huge number participated in physical verification except field students who will be visted at their field places.

On their side loan beneficiaries students showed their satisfaction in the whole process and gave the huge cooperation to the University and HESLB from beginning to the end of verification.

Hussein Ndawaine a Bachelor of education in Mathematics( BED-MATH) first year student said that it is good for HESLB to conduct such verification so as to recognize who receive loan wrongly in order to give those who are qualified and missed it.

“You know there are students who receive loan while are unqualified they replaced poor qualified students in the street. They were deprived loan because of this unqualified ones if they are recognized they will leave those chances to the poor students” said Ndawaine.

According to HESLB officers the result of physical verification of HESLB loan beneficiaries will be provided nationwide after all universities in the country being verified.

 

MUHIMU SANA MAOMBI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU 2016/2017. SOMA HAPA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Inapenda kutoa taarifa kwa Umma na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 Julai 2016.

Katika kipindi hicho waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku uliopo kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo kwa njia ya mtandao.

Utoaji wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya 16 na 17.

Kwa taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya kuomba mikopo ni Julai 31, 2016.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.


Friday, 24 June 2016

SWIMMING THE GOOD SPORT FOR YOUR HEALTH,FEATURES ARTICLE FROM ST.AUGUSTINE MWANZA TANZANIA.




By GEOFREY MICHAEL KAMAGHE

Swimming is a well-known sport which has its roots in Britain during the period of 1830 were it was part of the Olympic games in the year 1986. Swimming was taken a serious sports after a lot of people had interest on the game at first the only swimming style used was the breaststroke
The funny thing about swimming is that animals are naturally born with swimming ability naturally but the complexity comes to human beings who they need to learn so that one can be able to swim perfectly and not drown in the water and that is why many people are afraid of water and practising swimming activity
People ask question why should they learn to swim?  The answer to this question is “YES!” everybody should learn how to swim for the sake of safety leaving behind the fact that is a sport but also everybody should learn swimming since it’s a good physical exercise  to conduct, since ones all body parts work together and making them physical fit.
Most doctors agree that swimming is a healthy form of exercise. It requires you to use many of the muscles in your body, is for building strength and endurance and is beneficial for your metabolism and your cardiovascular. The water provides a natural resistance when your swimming .While also making the activity strenuous on your body. Water in most cases, also provides a natural cooling element or the body.
The following are some of the importance and benefit of swimming to human beings, these are as follows. First, the psychological benefits of swimming arewhen one has a swim session in a pool there he or she relaxes the mind, uplifts the spirit and its also often an occasion for social contact.
Secondly, for one to be able to swim can be able to attain several jobs such as life guards, fisherman and professional divers. Also being able to swim will open up a lot of recreational possibilities that would not be safe to practise if one doesn’t know how to swim these are like; surfing and boat fishing.
The best exercise to burn up calories in the body easy and reduce up the body quickly is the swimming exercise, the work out itself can help you to burn up all over 800 calories per hour for the laps you will take during a normal swimming.
If you are a resident of Mwanza and interested in swimming lessons and you do not know the location for the pools, these are several areas where you can learn the activity, in Malaika Hotel at ilemela district, Adden Palace Hotel at Pasiansi area and near Malimbe famously known as Fisheries.
So my dear friends, for a healthy and great body start swimming lessons if you are an expert and you have not yet start the work out then you have get a picture on the importance of swimming take it a serious issue for betterment of your body physic and health as well.

Thursday, 23 June 2016

BUSINESS ADMINISTRATORS ASSOCIATION FROM TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) THEY BRING TO YOU BBA LAUNCHING AND ENTERPRENEURIAL SEMINAR


BAA launching and entrepreneurial seminar which will be held at Tanzania Institute of Accountancy on this  Saturday at 10 am up to 2pm.
The main speaker Maida Waziri, President of voice of Women Entrepreneurs Tanzania and Managing Director of IBRA Contractors Ltd.






A retired president of Business Association Mr.Elisha Bernad (at the center) and his cabinet in a group phtoto .


They are showing a flies which show the description of the event which will be held at their institute on this Saturday.



All student at TIA  and near colleges your mostly invited at this event so as you can gain more experience and exposure.




 
 TIASO President (at the middle with jeans trouser) showing a support to the BAA Association on advertising their event.

For more story about this

  Umoja mpya wa wanafunzi wanaosoma uongozi wa biashara katika chuo cha Uhasibu Tanzania(BAA-TIA),wakishirikiana na kamati wezeshi wanatarajia kufanya semina ya ujasiriamali siku ya jumamosi ya tarehe 25 mwezi wa sita mwaka 2016 sambamba na kutambulisha rasmi umoja huo kwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho.
Semina na uzinduzi huu umekuja kama neema kwa wanafunzi wa vyuo vya juu hasa kwa  wanaomalizia masomo yao kwa mwaka wa tatu wa shahada,mwaka wa pili wa stashahada na wale wanaochukua astashahada katika chuo hiki cha uhasibu.
Umoja huu uliondwa kwa lengo la kuhamasisha elimu ya kujituma na uelewa halisi wa maswala ya biashara pamoja na kumpa uzoefu mwanafunzi husika katika fani ya uongozi wa biashara unategemewa kuleta matunda bora katika tasnia ya uongozi pamoja na kuimarisha mahusiano na taasisi zinginezo zinazofundisha masomo ya biashara.
Mgeni mzungumzaji mkuu katika semina hii anatarajiwa kuwa mama Maida Waziri mkurugenzi wa kampuni ya IBRA Contractors.
Hii imewezekana kufuatia ushirikiano wa wanafunzi pamoja na wakufunzi wanaofundisha masomo ya ujasiriamali shuleni hapo wakiongozwa na mkufunzi mama  A.Lauwo,Mwenyekiti mwezeshaji Ndugu Gwamaka Andrew,Alex Mujwahuzi kama Katibu Mwezeshaji, kiongozi wa darasa Lidya Ndomba ,Theresia Chacky,Richard Mwakatumba,Imelda Mitti pamoja na Irene Mbura
 Kuhusu Umoja wa wanafunzi wa Masomo ya biashara
Umoja huu ni umoja mpya kabisa kwa chuoni hapo ambapo kabla ya kupata viongozi wa kutoka madarani ulikua chini ya kamati ya darasa la wanafunzi wa mwaka wa tatu.
Wanafunzi hawa wanaokaribia kumaliza mwaka wao wa masomo walianza jitihada zao hizi za kuanzisha umoja huu wakiwa mwaka wa pili ambapo kamati iliundwa na wanadarasa kukamilisha zoezi kamili.
Kamati hii ilikua na mwenyekiti ndugu Elisha Benard, msaidizi wa mwenyekiti Maryam Seif, katibu Peter Charles ,msaidizi wake Irene Mbura na Muhidini Mdanku kuwa mweka hazina.
Pamoja na hao kamati ilichagua wapangaji matukio ndugu Alex Mujwahuzi na bi Grace Semagoda, viongozi wa darasa Bi.Consolata Mayokolo na Bw. Albert Washenta walichaguliwa kuwa wahamasishaji wakuu kwa nafasi zao kama wawakilishi wa darasa.
Ndugu Jeremiah Ngalla alichaguliwa kuwa mkuu wa kitengo cha Tekinolojia Mawasiliano akiungana na Gabriel Lucas,Jimmy Wilbert,Yusuph Kaseko,Yusuph Idd na Othmani Panyika.
Wajumbe wengine Katika kamati hii ni Jaquiline Mwayole,Godfrey Balyo,Samweli Ngwavi,Diana Muganyizi,Emanuel Chagoha,Maimuna Anjechele,Martin Bayona ,Shabani Jumapili,Josephine Joseph na Michael Ngosha.
Kamati hii waanzilishi waliweza kuandaa katiba iliyopitiwa na mwanasheria wa chuo Bw.Mayunga na kuruhusiwa kuendelea na zoezi la kupata uhalali kutoka ngazi nyingine za chuo.
Kamati iliwakilisha barua ya maombi kwa Mkuu wa Idara ya Masomo ya uongozi wa biashara na Masoko Bw.Lucas Ng’webeya ambaye alipenda kazi iliyofanya na kamati hii na kuahidi ushirikiano kutoka kwake.
Barua rasmi ya kuomba kutambuliwa na uongozi iliandikwa kwenda kwa mkuu wa chuo na kukubaliwa kuendelea na zoezi la kuutangaza umoja na kufanya zoezi la uchaguzi.
Tarehe 22 mwezi wa Sita , Umoja huu ulifanya uchaguzi wake wa Awali na kupata viongozi wake Mwenyekiti William Msemo,msaidizi wake Seleman W. Selemani, katibu wa umoja Singizi Hassani na msaidizi wake Shokolo Kashindye.
Bi Halima Salehe Machalina alichaguliwa kuwa mweka hazina wa Umoja huu,uchaguzi huu ulienda sambamba na kuchagua wawakilishi wa madarasa waliongia katika vitengo vya Tekinolojia Habari , Mawasiliano na uenezi, itifaki na katiba pamoja na kitengo cha mipango.
Walioingia kwenye kamati ya Tekinolojia Habari ni ndugu Daniel O.Lyamula, Ramadhani Mohamedi na Rogers Alex.
Edward Albert, Hafsa Abdi Mjaka ,Scholastica Mdee ,Omari Sufiani na Winton Elia waliingia kitengo cha habari na uenezi wakati ndugu Selemani W.Selemani ,Hassani Singizi,Samweli Elias na Kafumu John wakiingia kitengo cha katiba.
Athanasio William,Ally J Juma, Fatma Shabani na Joyce Zephania walifanikiwa kuchaguliwa na wajumbe kutoka madarasani kwao katika kamati ya mipango ya Umoja huu.
Kamati ya uwezeshaji na kamati Anzilishi ya umoja wa wanafunzi wa masomo ya biashara unawakaribisha wote katika tukio hili jema.



Wednesday, 22 June 2016

SPORTS ARTICLE FROM ST.AUGUSTINE UNIVESRITY IN MWANZA


THERE IS LIFE AFTER BASKETBALL, STUDY HARD.
BY GEOFREY MICHAEL KAMAGHE
On the Saturday 28th last week a splendid match between the St. Augustine alumni versus the modules who are the student continuing with studies, team alumni were the one who finished victorious by 71 – 70 baskets.
The game started during 1600 hours and both team modules and alumni were greedy on being the winner of the game with a strong and tough warm-up, though the alumni were small in number but still they managed to play a tough game.
The first quarter of the game showed the alumni a different picture towards team modules since the team modules lead the quarter by 17-11, at the moment the alumni were patient studying the game and due to small number of substitutions the alumni play a very slow but making sure of getting a basket on each ball they gate.
The second and the third quarter as well was tough and still the team modules maintain their leading positions but it was not all about speed and strength but also experience of the game was needed for them to maintain their position, poor substitution by the modules made them into unnecessary turnovers which were well used by the alumni, and till the third quarter the scores were 57- 47 team module leading the match.  
The amazing play by Chelu Mapolu, the alumni big man and defender made it difficult for the team modules to play a good defense since Chelu trapped the modules tem big man into foul trouble and making the game tough for modules to defend attacks from their brothers Alumni.
On the last quarter the game gain momentum after a tie in the last two minutes of 69-69 and there is when the alumni left behind the modules, though the modules player Frank Sele and Romanus Kissia missed out the free throw which if they could make them right they could change the reslts but the players fail to control the game pressure as it was not there lucky day.
On the close down, the alumni acting coach Benson Nyasebwa said, “you should take the game serious and win it when you had a chance since your first line was not strong enough, you had strong players and still you hesitate, next time it’s not a must for every player to play since what we want is victory and nothing else.”
The SAUT team modules captain Mrumbi Issa thanked the alumni for the time since they had various jobs to do but they took the call immediate as the team needed and added that,” I ask for this not to be the end of the plays, we should take it as a behavior for you to remember the life as students and advising us on the real image of life out the bars of university”


Tuesday, 21 June 2016

Shirika la viwanda vidogo vidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa morogoro watoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa SUA



Shirika la viwanda vidogo vidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa morogoro watoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa  (SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA) 
Na Asnain Chionda,Morogoro


Shirika la viwanda vidogovidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa morogoro wametoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa shahada ya sayansi na teknologia ya chakula wanaosoma katika chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Mtaalamu wa teknologia ya chakula katika shirika hilo Bi Joan Steven,aliwaeleza wanafunzi hao umuhimu wa kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao badala ya kukaa nyumban muda mrefu kusubiria kuajiriwa.Pia Bi joan aliwaeleza wanafunzi hao kuhusu shughuli zinazoendeshwa na shirika hilo na kuwahimiza wanafunzi kujijengea mazoea ya kutafuta ujuzi katika mashirika kama sido ili waweze kujiajiri wenyewe katika viwanda vidogo,aidha Mtaalamu huyo aliwaeleza wanafunzi hao juu ya mikopo midogo midogo inayotolewa na Shirika hilo na kuwataka wanafunzi na watu wengine kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo yenye lengo la kuwawezesha wajasiliamali wadogo nchini Tanzania

FURSA KWA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA ZAIDI SOMA HAPA


Sunday, 12 June 2016

WANAFUNZI WA KITIVO CHA SHERIA WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI) WAFANYA SHEREHE YA KUAGANA JIJINI DAR ES SALAAM.

Wanafunzi wanao soma sheria chuo kikuu cha Dar es salaam,wakiwa katika sherehe ya kuagana kabla ya kufanya mtihani wa mwisho,baada ya kusoma kozi hiyo kwa miaka mnne hapo chuoni.

 Katika mapozi tofauti tofauti

 Hii ni keki yenye nembo ya chuo kikuu cha dar Dar es salaam,kuashiria wanatambua umuhimu wa chuo chao.

  picha ya makundi ya wanafunzi hao katika sherehe hiyo iliyo fanyika jijini Dar es salaam.

 


 Wana sheria watarajiwa wakiwa katika ubora wao katika shughuli hiyo. 
 Huyu ndio Mtaalamu wa Sheria za Keki pale chuo kikuu cha Dar es salaam,katika ubora wake.

Friday, 10 June 2016

HELLEN, MTANZANIA ALIYETAJWA NA FORBES KUWA BILIONEA AJAE


Jina lake ni Hellen Dausen na umri wake ni miaka 29 ( November 1986) na aliipiga chini ndoto yake aliyokaa nayo miaka kumi bila kumfanikisha kisha akaingia kwenye mbio za Ubilionea na kitu kingine kabisa maishani mwake.
Unaambiwa Jarida la FORBES ambalo limekua na nguvu duniani na kutoa ripoti mbalimbali zikiwemo za uchumi na watu na utajiri wao, lilikua na list ya idadi ya vijana takribani elfu mbili lakini Hellen akaibuka miongoni mwa vijana 30 wa Afrika wenye fikra na mikakati ambayo ni utajiri wa siku chache zijazo.
Ishi ndoto zako kijana.

NAIBU WAZIRI WA MAZINGIRA NA MUUNGANO MGENI RASMI TAMASHA KUBWA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

Katika kutengeneza Msingi mzuri kwa wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya inafanya Maonyesho Makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku ya tarehe 11 June 2015.
Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira wamealikwa kutoa mada na kuonyesha uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walioalikwa kwenye Tamasha Hilo ni; Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba amba ye ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wakujitegemea na mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – MenejawaTawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo ni Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.LuhagaMpina.
Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.

USIKOSE KESHO KWENYE ELIMIKAWIKIENDI KWENYE UKURASA WA TWITTER TUJUMUIKE WOTE KESHO.


Tukielekea maadhimisho ya wa Afrika, kupitia italeta mjadala wa

Wednesday, 8 June 2016

Wanafunzi wa darasa la Saba waaswa kuongeza bidii katika masomo ya Sayansi

 Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.

Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi  matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha

 
Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi


Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.

Wito  huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.
Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).

Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.

Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi  kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.