Shirika la viwanda vidogo vidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa morogoro watoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa (SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE (SUA)
Na Asnain Chionda,Morogoro
Na Asnain Chionda,Morogoro
Shirika la viwanda vidogovidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa morogoro wametoa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi wa shahada ya sayansi na teknologia ya chakula wanaosoma katika chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Mtaalamu wa teknologia ya chakula katika shirika hilo Bi Joan Steven,aliwaeleza wanafunzi hao umuhimu wa kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao badala ya kukaa nyumban muda mrefu kusubiria kuajiriwa.Pia Bi joan aliwaeleza wanafunzi hao kuhusu shughuli zinazoendeshwa na shirika hilo na kuwahimiza wanafunzi kujijengea mazoea ya kutafuta ujuzi katika mashirika kama sido ili waweze kujiajiri wenyewe katika viwanda vidogo,aidha Mtaalamu huyo aliwaeleza wanafunzi hao juu ya mikopo midogo midogo inayotolewa na Shirika hilo na kuwataka wanafunzi na watu wengine kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo yenye lengo la kuwawezesha wajasiliamali wadogo nchini Tanzania
Asantee...
ReplyDeleteKaribu na tunashukuru kwa kututumia habari yenye ueledi katika taifa letu!unakaribishwa kukutumia tena.
Delete