Friday, 10 June 2016

NAIBU WAZIRI WA MAZINGIRA NA MUUNGANO MGENI RASMI TAMASHA KUBWA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA

Katika kutengeneza Msingi mzuri kwa wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya inafanya Maonyesho Makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku ya tarehe 11 June 2015.
Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira wamealikwa kutoa mada na kuonyesha uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walioalikwa kwenye Tamasha Hilo ni; Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba amba ye ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wakujitegemea na mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – MenejawaTawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo ni Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.LuhagaMpina.
Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment