Thursday, 27 July 2017

SERIKALI YAPIGILIA MSUMARI UDAHILI

 
BAADHI ya vyuo vilivyosimamishwa kufanya udahili katika baadhi ya programu zake, vimebainisha kuwa vimeanza kuchukua hatua ya kuondoa dosari hizo, na viko tayari kufanyiwa uhakiki tena.
Hayo yamebainishwa jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 12 ya Taasisi za Elimu ya Juu nchini yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri, Thadeus Mkamwa alikiri kuwa baadhi ya matawi ya chuo chake, yamesimamishiwa udahili katika baadhi ya programu zake, lakini ni kutokana na tatizo la mawasiliano baina ya chuo hicho na TCU.
“Ni kweli walituletea notisi ya siku 14 tujibu kuhusu upungufu waliobaini, tumewajibu mapema tu, lakini wakati tunasubiria matokeo, tukasikia kwenye vyombo vya habari kuwa, baadhi ya programu zetu zimesimamishwa zisifanyiwe udahili, lakini tunalifanyia kazi,” alisema Mkamwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu nchini. Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Vyuo Vikuu vya Kanisa Katoliki, Atunus Simwambi, alikiri kuwa programu iliyosimamishiwa udahili ilikuwa kwa muda wa miaka mitatu angu ianzishwe haijawahi kuwa na wanafunzi na hivyo kutofundishwa chuoni hapo.
“Programu hii ilianzishwa kwa ajili ya watu wanaotakiwa kuwa mapadri au wanaokwenda kufanya kazi za utume katika maeneo mbalimbali. Kwa kuwa kuna mchakato wa kuunganisha chuo chetu na Chuo cha Filosofia cha Kibosho, tulitarajia programu hii itarejea,” alisema. Chuo hicho kimesitishiwa programu moja ya Bachelor of Arts in Philosophy with Ethics. Naye Makamu wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Profesa Hamza Njozi, pamoja na kukiri kuwa katika baadhi ya programu zilizosimamishwa udahili zilikuwa na changamoto ya walimu, alieleza kuwa dosari hizo zimefanyiwa kazi kama ambavyo Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilivyoagiza katika notisi yake ya siku 14.
Alisema chuo hicho kilipatiwa notisi ya siku hizo 14 inayoanzia Julai Mosi hadi 14, mwaka huu, kufanyia marekebisho dosari hizo, lakini hata baada ya kutoa majibu, walishtukia kupitia vyombo vya habari, kuwa programu hizo zimesimamishiwa udahili. Akizungumzia taarifa ya TCU, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Watoa Elimu Wasiotegemea Serikali Kusini mwa Jangwa la Sahara(CIEPSSA), Benjamin Nkonya alisema uamuzi huo wa serikali ni nzuri kwani una nia njema ya kurudisha heshima ya elimu nchini.
Nkonya alisema hatua hiyo inapaswa kuungwa mkono na wadau wa elimu nchini kwa sababu yapo baadhi ya mambo ambayo yamechangia kiwango cha elimu kushuka wakiwemo baadhi ya wasomi ambao wameonesha udhaifu kwenye utendaji wao. “Kwanza kabisa tunaona jinsi rais anavyokerwa na baadhi ya wasomi ambao wanavuruga nchi badala ya kuwa kioo, ameona hakuna mwelekeo nah ii inawezekana ikatokana na mfumo wa elimu ambao wakati mwingine baadhi ya shule au vyuo vimetoa elimu isiyokidhi, sasa tunapojisahihisha ni vizuri ili tuwe na mfumo thabiti kwa manufaa ya taifa,” alisema Nkonya.
Alisema kwa bahati nzuri sekta ya elimu nchini kwa sasa imepata mtu sahihi kwenye wizara hiyo inayoongozwa na Profesa Joyce Ndalichako ambaye hata wao wana imani ataendelea kuiboresha zaidi kwa sababu utendaji kazi wake unatambulika. “Profesa Ndalichako ni mtu makini, nakumbuka nilipokuwa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo Vya Serikali (TAMANGSCO) zaidi ya miaka 10, Profesa Ndalichako alipokuwa NECTA, aliadhibu shule au vyuo vilivyokosea, na alitoa adhabu kali hata wakati mwingine kufutia matokeo shule nzima alipobaini udanganyifu, alifanya hivyo kulinda heshima ya elimu,” alisema Nkonya. Hivyo akashauri kuwa uamuzi uliofikiwa na serikali kupitia TCU ni uamuzi sahihi na kuvishauri vyuo husika kufuata maelekezo ili kuhakikisha kiwango cha elimu kitolewacho kina ubora unaotakiwa.

Monday, 17 July 2017

Ulemavu sio mwisho wa kutimiza ndoto, mapacha walioungana watusua kielimu



Maria na Consolata ni wasichana waliozaliwa wakiwa wameungana na sasa wamekuwa na furaha kubwa baada ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita.
Mapacha hao wenye umri wa miaka 19 walikuwa wanasoma katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa nchini Tanzania, wamefaulu kwa kupata daraja la pili katika masomo yao ya kidato cha sita na kuwa na matumaini kuwa ndoto yao ya kuwa walimu hapo baadaye inaelekea kutimia.
“Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana,” amesema Consolata.
Baada ya matokeo hayo, Maria na Consolata wamesema kuwa wanapendakuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika chuo kilichopo katika mkoa wanaoishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao wangependa kubadili mazingira, hivyo wamechagua Chuo Kikuu Cha Ruaha.
“Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi,” alisema.
Kadhalika, mapacha hao wamesema wamechagua kubakia mkoani kwao kwa sababu ya hali yao, wamesema hawatamudu kuishi kwenye mazingira ya joto. “Mji wa Iringa ni baridi, hali hii tumeizoea.”
Aidha, wametoa wito kwa wazazi, wamesema hakuna linaloshindikana iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu, wawaone kama watoto wengine na kuwapa mahitaji yao ya msingi, wawawezeshe, wawapatie nafasi ya kujiendeleza maana wakiwezeshwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.
” Wazazi washukuru Mungu kupata watoto wenye changamoto kama wao wasione kuwa na mtoto mlemavu ni laana.”

Saturday, 15 July 2017

START UP GRIND DAR HOSTS GODFREY MAGILA

 
Godfrey Magila is the founder and CEO of Magilatech, a software development and security auditing company in Dar es Salaam, Tanzania started in 2012. 
Magilatech launched Tigobackup, a mobile security application performing full content backup on mobile device and antitheft commands. The app has recovered more than 3,600 lost and stolen devices. 
Through his company, Magila employs 14 people, has seven contract employees, made over $1 million last year, has app contracts with Airtel, Vsomo, Maxcom, Selcom and DayOne Softcom. Magila holds a Bachelor of Finance and Accounts degree and is a self-taught programmer. He is also an entree into Forbes Africa 30 Under 30, 2017
 
DON'T MISS IT

POLENI KWA USUMBUFU.....LINK MPYA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2017 IPO HAPA KWENYE BLOG YENU PENDWA KARIBUNI SANA.

 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita. 

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
 
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

 Bonyeza HAPA kufatilia matokea ya shule zote Tanzania.
BONYEZA LINK HII HAPA CHINI


Tuesday, 31 January 2017

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

 
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
 
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

==>>Bofya  <<HAPA>  Kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne 2016



Monday, 30 January 2017

MTANZANIA PEKEE AINGIA KWENYE SHINDANO LA DIGITAL PITCH COMPETITION.

 
Julius J. Julius ni Mtanzania Pekee alieingia kwenye mashindano ya DIGITAL PITCH COMPETITION ambayo yantarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini,kijana huyu ndiye anayewakirisha nchi ya Tanzania peke yake.Basi kama Mtanzania unaombwa kumpiga kura kadri uwezavyo ili aweze kuipeprusha Bendera ya Tanzania.
Jinsi ya kupiga kura bonyeza hapa  http://woobox.com/t7kzv8-cpk/gallery/SWEgB8FnaAg
 kisha unakuwa umeshampigia kura huyu kijana waKITANZANIA na unaweza kurudia kupiga baada ya masaa sita tena.Tuonyeshe uzalendo kwa kumsaidia kijana huyu.

Friday, 27 January 2017

ASASI YA HIFADHI YA JAMII KUTOKA IFM (ISPA) YA FANYA DHIARA YA KIMASOMO KWENYE MMAMLAKA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM.



 Asasi ya Hifadhi ya jamii kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha Ifm,leo hii waitembelea mamlaka ya hifadhi ya jamii,ili kujifunza kwa vitendo jinsi mamlaka hiyo inavyo fanya shughuli zake za kuisimamia secta ya hifadhi ya jamii hapa nchini,wanafunzi hao ni ambao wanasoma fani ya uifadhi wa jamii ambayo inatolewa hapo chuoni kwao.


Makamu wa Rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii ndugu Carolyn Mmari akiongoza wanafunzi wenzake wakati wakujipatia chakula.

  




 Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na furaha baada ya kufika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi ya jamii leo hii jiji Dar es salaam.


Mkurungenzi wa sharia katika Mamlaka hiyo akiwakaribisha wanafunzi hao kwa niaba ya Mkurungenzi mkuu.


 
 


 
Mmoja ya wanafunzi pamoja na afisa wa mmalaka ya hifadhi ya jamii wa kifatilia kwa umakini semina ikitolewa na afisa wa mamlaka ya fidhai ya jamii.
 

 Rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii Bwana Sylvester Dionizy kutoka chuo cha usimamizi wa Fedha IFM,akitoa neno la shukrani kwa Mamlaka kupokea wito wao wakuja kujifunza hapo ofisi kwao.


 Afisa wa Mamlaka ya hifadhi ya jamii akishukuru ushiriki wawanafunzi kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) na kutambua umuhimu wa watalam wa Hifadhi ya Jamii Katika Nchi yetu.
 
 

 Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Asasi ya Hifadhi ya Jamii na maafisa wa mamlaka ya Hifadhi ya jamii.

Saturday, 21 January 2017

Start Up Grind Dar is starting the year with a BANG by hosting Faraja Nyalandu.


Faraja Nyalandu is a lawyer turned tech-preneur and founder of Shule Direct, a learning and revision platform for secondary school students in Tanzania. Shule Direct produces high quality digital learning content specifically designed around the Tanzanian National Curriculum and building an adaptable platform to make this content available on a range of devices from the most basic mobiles to full-featured desktop learning portals.
Don't Miss out Faraja Nyalandu on 25th January at Buni Hub from 18 Hours to 21 Hours
Buy tickets online via bit.ly/2juv3FM for only 8,000 Tshs
Tickets at the Gate; 10,000 Tshs
Be Awesome by sharing with your friends

Tuesday, 30 August 2016

WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA KUNUFAIKA NA MO SCHOLARS PROGRAM





Taasisi ya Mo Dewji (Mo Dewji Foundation) inatoa udhamini kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo ya elimu ya juu kwa miaka minne katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM). Udhamini huo utakaojumuisha malipo ya ada, vitabu, ada ya maktaba ya kusomea, malazi na chakula kwa muda wote utakaokua katika masomo ya shahada yako.

Kwa taarifa Zaidi kuhusu jinsi ya kujiunga pamoja na vigezo vyake, tembelea katika ukurasa wa MO Dewji

Wednesday, 10 August 2016

HE KPMG INTERNSHIP CHALLENGE 2016 TO ALL SECOND YEAR STUDENTS





HE KPMG INTERNSHIP   CHALLENGE 2016
BIR II & BSP II are hereby invited to Essay writing competition that is organized by Tanzania Insurance Brokers Association (TIBA), KPMG and the Faculty of Insurance and Social Protection-FISP IFM.

Main Theme:  “How to achieve excellence in the Tanzanian Insurance Sector in/on:

(i) Agriculture
(ii) Micro-Insurance
(iii) Local Content

You can choose a single topic or multiple topics, however, each topic (if Multiple topics are chosen) are to be submitted independently and will be evaluated independently.

Qualifications:
a) IFM Students Only
b) 2nd year of Study
c) Social Protection/Insurance and Risk Management

Prize for Winning Student:

a) Internship with KPMG for 6-12 months
b) Decent sized facilitation from KPMG, a monthly sub fee and a Samsung Tablet for the winner
c) Featured in the KPMG global Magazine
d) Paid trip to Zanzibar- 2 nights stay at sea Cliff Zanzibar Resort and awarded at TIBA Annual conference

Duration of competition:
a) Effective from 3rd August 2016
b) Last submission accepted on 5th September 2016
c) Email submissions to be sent on: ifmintern@kpmg.com
d) Winner will be notified by 15th September 2016

Number of words- a minimum of 1200 with a maximum of 1,500

For clarification, please contact the office of the Dean-FISP

Issued by the Office of the Dean-FISP
 

Friday, 5 August 2016

BREAKING NEWZ!!!MABWENI YA SHULE YA SECONDARY LONGIDO JIJINI ARUSHA YA WAKA MOTO.


LONGIDO INAUNGUA MOTO JAMANI SASA HIVII TUWAOMBEE WANAFUNZI KWA SABABU WAMEZIMIA WENGI WANAPELEKWA HOSPITALINI HAKUNA WAKUOKO
Huu ujumbe umetumwa na Mmoja wa ripota wetu kutokea jijini Arusha.



Kaa nasi kwa habari zitakazo Jiri katika shule hiyo.

Tuesday, 2 August 2016

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI JIJINI DAR LEO




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified" Mjema alizindua uwanja huo leo katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate akishuhudia tukio hilo.




Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo.



Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo. 


Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto) akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified" uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa. 

Kwa habari zaidi
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya "Be Kidotified". Alisema kuwa amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya kuendeleza michezo na taaluma.
Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli) kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.
 

Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi milioni 50.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
 

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo vitamwezesha mshiriki kupata ajira. Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.
 

Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo, lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi. “Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ”
 

“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation, na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate. Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.
 

Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.

Habari kwa Hisani ya Michuzi

Friday, 22 July 2016

WANAFUNZI WA SUA WALITOKA SJUIT WAPIGA KAMBI BODI YA MIKOPO.




Na Asnain Chionda JR.



 
Wanafunzi wanaosoma katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) Waliohamishiwa na Serikali chuon hapo wakitokea chuo kikuu cha mtakatifu Joseph tawi la Songea,  Leo wamepiga kambi katika bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (Heslb) wakishinikiza bodi hiyo kuwalipa pesa zao za kujikimu walizocheleweshewa kwa kipindi cha Miezi minne. 
Wanafunzi hao ambao wanasoma chuon hapo wameshindwa kuendelea kuvumilia kukaa chuoni hapo kwa ahadi za kila siku kutoka bodi hiyo.
Aidha, wanafunzi hao ambao wameamua kupanda basi kutoka Chuon kwao Morogoro had Dar es salaam zilipo ofisi hizo, wamesikitishwa na kitendo cha bodi ya mikopo kutokuwajali na kushughulikia matatizo ya wanafunzi hao kwa muda huo wote tangu walipowasili chuoni hapo mapema mwezi wa Tatu mwaka huu hali iliyowalazimu wanafunzi hao kupiga kambi ofisini hapo.
Hadi kufikia muda ambao taarifa hizi zinapelekwa kwenye mitambo ya Scholars Blog,  wanafunzi hao bado wapo katika ofisi za bodi hiyo wakisubiri mrejesho kutoka kwa mtendaji mkuu wa bodi anaehusika na utoaji wa pesa hizo kwa wanafunzi ambae ameahidi kushughulikia Suala hilo haraka iwezekanavyo.


 
 
 
 
 
 








Afisa wa Bodi ya Mikopo akitoa maelekezo kwa wanafunzia hao.



Sunday, 17 July 2016

TCU YATOA UFAFANUZI JUU YA UDAILI WA WANAFUNZI KWENDA VYUO VIKUU.

Tume ya vyuo vikuu (TCU) imetoa ufafanuzi kuhusu alama zitakazowezesha mwanafunzi kudahiliwa Chuo Kikuu baada ya kuchanganya wengi.

Yasema inatakiwa mwanafunzi awe na principal pass mbili walau zifikie point 4 kwenye masomo mawili na si lazima ziwe D mbili.


Monday, 11 July 2016

WAZIRI ATEMBELEA BANDA LA PSPF


Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Angelina Mabula, (kulia), akimsikilzia AfisaMasoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mgire Werema, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwnye viwanja vya Mawlimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia Mpango wa PSS, Fatuma C. Luwago, kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,

 Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania, (TANTRADE), Theresa H. Chilambo, (kushoto), akijaza fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa hiari kwenye banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa , Dar es Salaam, Julai 8, 2016. Anayemuhudumia ni Joseph Lyimo, kutoka kitengo cha Mawasiliano PSPF.


Afisa Huduma kwa wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Judith Mtweve, (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 8, 2016



 Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,