Saturday, 31 October 2015
Tuesday, 27 October 2015
WANAFUNZI 65 KUONDOKA KWA MASOMO NCHINI CHINA
WANAFUNZI 65 KUONDOKA KWA MASOMO NCHINI CHINA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza
na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China,leo jijini
Makao ya Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Link Education (GEL),Abdulmaalik Mollel akizungumza
na wazazi na wanafunzi wanaotarajia kuondoka Oktoba 28 kwenda kusoma
masomo ya elimu ya juu yalifanyika makao Makuu ya GEL leo jijini Dar es
Salaam.
Wazazi na Wanafunzi. wakimsikiliza Abdulmaalik Mollel
Sehemu
ya wazazi na wanafunzi wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya
juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education
(GEL),Abdulmaalik Mollel hayupo pichani leo makao makuu GEL leo jijini
Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje leo jijini Dar es Salaam.
Watoto wanaotoka familia maskini Longido
Watoto wanaotoka familia maskini Longido washindwa kuhudhuria masomo.
Asilimia
kubwa ya watoto wanaotoka katika familia maskini wilayani
Longido mkoani Arusha wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na
changamoto zinazowakabili wazazi wao likiwemo tatizo la njaa,ukosefu
wa huduma ya maji,na Afya.
Wakizungumza wakati wanapokea msaada wa zaidi ya milioni 230
zilizotolewa na mfuko wa Tassaf baadhi ya wananchi wa vijiji
vinavyokabiliwa na matatizo hayo pamoja na kuushukuru mfuko wa
Tasafu wamesema ukosefu wa huduma za kijamii bado ni janga kubwa
kwao na watoto wao.
Baadhi ya viongozi wamesema pamoja na kusisitiza wazazi
kupeleka watoto wao shule wanatembea umbali mrefu na wanapofika
shule wanasinzia badala ya kumsikiliza mwalimu na jambo lililoko
wazi kuwa hawataweza kufanya vizuri.
Wakikabidhi fedha hizo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
longido bw.Felexs Kimario na watendaji wa Tasaff wamesema vijiji
27 vimefikiwa na mpango huo na kaya 259 zimepatiwa msaada huo
ambao ni kwa ajili ya kusaidia elimu afya na kujikimu.
Longido ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Arusha zinazokabiliwa
na tatizo kubwa la ukosefu wa huduma za kijamii ikiwemo
maji,miundombinu ya elimu na Afya.
MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA
MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K'NJARO
Baadhi
ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya
kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani
Kilimanjaro.
Baadhi
ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la
kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada
wa Mo Dewji Foundation
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame
uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini.
Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao
kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule za umma
ambazo hazina ubora.
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
Mratibu
wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia
matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji
Foundation.
Friday, 23 October 2015
ELIMU YA STADI ZA MAISHA KUOKOA KUNDI KUBWA LA VIJANA WALIO NJE YA SHULE
Afisa
vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.
Godfrey Massawe (aliyesimama) akifuatilia majadiliano ya wawezeshaji
kitaifa wakati wa kazi za kikundi kwenye Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi
za Maisha yaliyofanyika Kanda ya Ziwa.
ILIGUNDULIKA
kuwa ulimwenguni kote na hususan nchini Tanzania, Vijana walio nje ya
shule ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa
yanayoenea kwa njia ya ngono, VVU na UKIMWI kwa kutokuwa na taarifa na
stadi za kuwaongoza hivyo kupoteza kundi kubwa la vijana ambalo ni taifa
la kesho.
Ufumbuzi
wa tatizo hili umeweza kufanyika kwa kuwapa vijana stadi za maisha
zenye upeo mpana wa maarifa na stadi zinazoweza kuwasaidia vijana
kuendana na mazingira shindani yanayobadilika.
Stadi
za maisha ni moja kati ya mikakati iliyobainika kuleta mabadiliko ya
tabia za mtu. Stadi hizi uhusisha stadi na uwezo wa kujenga tabia njema
ili kuepukana na matatizo yaliyopo katika maisha ya kila siku.
Mkabala
wa stadi za maisha unalenga katika kuendeleza na kukuza stadi
zinazoitajika katika mahitaji ya maisha ya kila siku kama vile
mawasiliano, kufanya maamuzi, fikra, kuhimili mihemko, uthubutu, ujenzi
wa kujiamini, kuzuia shinikizo rika pamoja na mahusiano.
Mkabala
huu pia unashughulikia ukuaji wa mtu ili awe na stadi za kumwezesha
kutumia aina zote za taarifa kuhusiana na masuala kama vile magonjwa ya
ngono, VVU na UKIMWI.
Mahitaji
ya stadi za maisha miongoni mwa vijana ni mengi na yanatofautiana baina
ya vijana wadogo na wakubwa, vijana walio nje ya shule na walio
shuleni, pamoja na walio na wasio katika ndoa hivyo kupelekea kuwa na
viwango vya mafunzo ya stadi za maisha vilivyopendekezwa na kubuniwa
kuwanufaisha vijana wasio mashuleni.
Wizara
inayosimamia masuala ya vijana imekua ikitoa mafunzo ya stadi za maisha
kwa vijana walio nje ya shule ili kuwapa vijana stadi za kukabiliana na
changamoto za kila siku katika maisha yanayowazunguka.
Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na shirika la
umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA)
wameweza kufikisha elimu ya stadi za maisha kwa wawezeshaji wa kitaifa
kutoka kanda ya Ziwa hivi karibuni ili kuweza kusambaza elimu hiyo kwa
vijana walio nje ya shule maeneo yote ya kanda ya ziwa hivyo kuwawezesha
vijana kukabiliana na dunia hii ya sasa ya sayansi na teknolojia.
Akifungua
mafunzo ya wawezeshaji kitaifa kutoka kanda ya Ziwa yaliyofanyika Mkoa
wa Mwanza hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga aliwataka wawezeshaji kitaifa wa stadi za
maisha kuwasaidia vijana kujitoa katika mitazamo hasi na kuleta
mabadiliko chanya katika jamii kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa
hili.
“Vijana
wakijiimarisha katika shughuli za kijamii na kiuchumi wataepuka
kuzungukwa na vihatarishi vya maisha kama vile VVU na Ukimwi, mimba
zisizotarajiwa pamoja na dawa za kulevya hivyo kujenga nchi kwa kutumia
nguvu kazi ya vijana” alisema Bibi. Nkinga.
Mafunzo
ya stadi za maisha yamekua yakiongeza hali ya kujiamini kwa vijana na
kutoa mbinu za kukabiliana na matatizo ya maisha kwa kuwapa vijana uwezo
wa kutumia muda wao kikamilifu kuzungumza na watu wasiowajua kuliko
ilivyokua hapo awali.
Aidha
Bibi. Nkinga alisema kuwa matarajio ya serikali ni kuona vijana wa
kitanzania wanajitambua kua wao ni nani, wanaenda wapi, na watafikaje
kwa kujua uwezo na udhaifu binafsi walionao ili waweze kupanga malengo
waliyonayo na kuyatekeleza kulingana na fursa zilizopo.
Vijana
wanaopata fursa ya kuwezeshwa katika stadi za maisha wameongeza viwango
vyao vya stadi za kujitambua na uwezo wa kuwasiliana na watu wa rika
zote hivyo kubadili tabia za vijana wa rika mbalimbali.
Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. James Kajugusi amesema kuwa kila kijana ana sifa za kujiunga
na mafunzo ya stadi za maisha zitakazowawezesha kukataa visingizio kama
vile umasikini, maradhi na masuala yanayoshauriwa na marafiki ambayo
yanaweza kuwaingiza katika vishawishi.
Bw.
Kajugusi amesema kuwa Mafunzo ya stadi za maisha yamelenga kupata
waelimishaji wa kitaifa wa stadi za maisha watatu kutoka kila mkoa
katika mikoa yote ya Tanzania bara ambao watawafikia waelimishaji rika
wa kila mkoa ili kuweza kufikisha elimu waliyoipata kwa vijana wa rika
mbalimbali katika Mikoa, Wilaya, kata, vijiji, vitongoji, mitaa, vijiwe
na sehemu rasmi za shughuli za vijana.
Stadi
za maisha zinaweza kuwekwa katika makundi matatu ambayo ni stadi za
maisha kwa ajili ya kujitambua, kwa ajili ya fikra na kwa ajili ya
mahusiano baina ya watu hivyo kwa pamoja aina hizi huweza kutoa majibu
kwa vijana kuwa wao ni nani, wanataka kwenda wapi na watafikaje hapo
wanapotaka kwenda.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru amesema kuwa vijana
waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao
kama watatumia vizuri uwezo walioupata katika mafunzo hayo watabadili
fikra za vijana wengi nchini hivyo kuweza kujenga taifa lenye afya
nzuri, weledi pamoja na ujuzi.
Stadi
za maisha humjenga kijana kufanya maamuzi sahihi hivyo kuondokana na
majuto na kumfanya kuwa huru katika kutoa maamuzi binafsi.
Kwa
kawaida stadi za maisha humpa kijana mwitikio wa uthubutu unaompa fursa
ya kusimamia anachotaka au anachoamini bila kumdharau au kuumiza
kihisia mtu mwingine.
Mtaalamu
wa masuala ya Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe amesema kuwa wawezeshaji
wa kitaifa waliopata Mafunzo ya Stadi za Maisha wana ari na motisha ya
kujifunza na kama wataendelea kuwa na ari hiyo watakua wabunifu na
wawezeshaji wazuri kwa vijana ndani ya jamii wanazoishi.
Aidha
Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Shinyanga Bw.
Ezra Manjerenga amesema kuwa vijana wa Mkoa wa Shinyanga wamekua
wakikabiliwa na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi hivyo ugeni wa mafunzo
ya stadi za maisha katika Mkoa huo utawavutia vijana wengi jambo ambalo
litapelekea kutimiza lengo la serikali kufikisha mafunzo hayo kwa
vijana wa rika mbalimbali.
Stadi
za maisha zinatoa fursa kwa vijana kupata taarifa za afya ya uzazi na
upatikanaji wa huduma ya afya ya uzazi, pia humpa kijana haki ya
kutambuliwa, kusikilizwa na kuheshimiwa utu wake bila kujali kiwango cha
elimu, hadhi yake au sifa nyingine itakayombagua na kumuweka katika
mazingira hatarishi.
Vijana
waliopata mafunzo ya stadi za maisha wamepewa dhamana na serikali
kwenda kuwatumikia vijana na kuhakikisha kuwa uhamasishaji wa mabadiliko
chanya miongoni mwao ili kuweza kuachana na tabia zote hatarishi na
kushiriki vyema kwenye shughuli za uzalishaji mali.
Serikali
inatambua kuwa vijana ni rasilimali muhimu kwa ajili ya ukuaji wa
uchumi na kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla hivyo kusimamia kwa
ukaribu zaidi elimu ya stadi za maisha kwa vijana wote nchini.
MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU YAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA JIJINI ARUSHA
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Mariado na walimu iliyopo Usa River ,wilaya ya
Arumeru mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu barani Afrika katika Mahakama ya
Afrika ya Haki za Binadamu iliyofanyika Oktoba 21 na kudai haki za
wenye ulemavu wa ngozi(Ualibino) kulindwa kama wananchi wengine.
Mwanafunzi
Kelvin wa shule ya Mariado akiimba wimbo Umoja wa Afrika(AU)ambao ni
maalumu wakati wa shughuli za umoja huo zinapofanyika.
Kamishna wa Tume ya Haki Binadamu na Utawala Bora,Zanzibar ,Mohamed Khamis Hamad akizungumza katika maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa kiingereza ya St.Jude ya Jijini Arusha wakiigiza athari za watoto wa kike kukeketwa.
Wanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa kiingereza ya St.Jude ya Jijini Arusha wakiigiza athari za watoto wa kike kukeketwa.
Wednesday, 21 October 2015
WANAFUNZI WA ST. JOSEPH WACHANGIA CHUPA 125 ZA DAMU MUHIMBILI
Balozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya akiwa na wanafunzi
wanaosoma kwenye shule hiyo hivi sasa. Kutoka kulia ni Benjamin Fred,
Maria Joseph na Vanessa Elieza Mwakila.
Mmoja
wa wanafunzi akichangia damu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuokoa
maisha ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH)
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya akitoa damu leo jijini Dar es Salaam katika shule ya St.
Joseph Cathedral High School zamani ikijulikana Shule ya Sekondari
Forodhani. Balozi Msuya ambaye alisoma kwenye shule hiyo mwaka 1975 ni
mmoja wa wanafunzi wa zamani waliojitokeza kutoa damu ili kuokoa maisha
ya wagonjwa wanaotibiwa Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
WANAFUNZI
waliosoma St. Joseph Cathedral High School zamani ikijulikana Shule ya
Sekondari Forodhani leo wamejitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
Watanzania ambao wanahitaji damu.
Wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo hivi sasa kwa kushirikiana na wenzao wa zamani wamefanikiwa kutoa chupa 125 za damu.
Akizungumzia
katika uchangiaji wa damu shuleni hapo , Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
Aminiel Aligaesha amesema suala la damu ni changamoto kwani hospitali
hiyo inahitaji wastani damu wa chupa 100 kila siku na kwamba kwa siku
hivi sasa zinapatikana chupa 24 hadi 40.
Alifafanua kwamba hivi sasa hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa wastani wa chupa 60 za damu kwa siku.
Kutokana na hali hiyo amewaomba
Watanzania kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
Watanzania kwani suala hilo linagusa maisha ya watu wote.
Ametaja makundi ambayo huitaji damu kwa haraka kuwa ni wagonjwa wa dharura, mama wajawazito, watoto na wagonjwa wa saratani.
Aligaesha amewashukuru
wanafunzi hao na wale wanaosoma hivi sasa kwenye shule hiyo kwa
kujitokeza kwa wingi kuchangia damu na kusisitiza kuwa kitendo
walichokifanya ni cha kuigwa.
Kwa upande wa wanajumuia
waliosoma shuleni hapo wamesema wameamua kujitokeza kuchangia damu ili
kuwahamasisha wanafunzi kuwa na utamaduni wa kujitolea katika jamii
jambao ambalo hivi sasa limefifia.
Aidha
kwa upande wa MNH imekuwa ikitoa matangazo mbalimbali ili Watanzania
wajitokeze kuchangia damu kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu kwenye
hospitali hiyo.
Katika
shughuli ya leo, Balozi Msuya alifika katika shule hiyo na kuchangia
damu kama walivyofanya wanafunzi wengine waliosoma hapo miaka 1950.
Balozi
huyo alisoma katika shule hiyo mwaka 1975, baadhi ya wanafunzi wengine
ni Mariam Zialora ambaye amesoma hapo 1964, Glen Dias mwaka 1954, Saada
Jaha mwaka 1970, Albertina Doarado mwaka 1968, Solomon Mihayo mwaka
1990, Tahir Othman 1990, Edith Mabena mwaka 1992, Edward Makwani mwaka
1970 na Ephrahim Tumwidike mwaka 2012.
Leo
wanafunzi hao wa zamani wameonyesha upendo wa hali ya juu kuungana na
wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo hivi sasa katika kuchangia damu.
Uamuzi huo wa wanafunzi hao wa zamani unapaswa kuigwa na shule nyingine
kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Shughuli
ya kuchangia damu leo imefanywa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa
kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).
Monday, 19 October 2015
AIRTEL KUPITIA MRADI WA TUNAKUJALI WAENDELEA KUSAIDIA SHULE HAPA NCHINI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akikata utepe kama ishara ya
kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya
Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya
Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Wanaoshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Priscilla Moshi (wa pili
kushoto), Mwenyekiti wa Shule, Mwemba Mwilima (wa tatu kushoto),
Wafanyakazi wa Airtel na watoto wa chekechea.
Wafanyakazi
wa Airtel wakifurahi na watoto wa Chekechea katika Shule ya Msingi
Kumbukumbu, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’,
lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi hao, kama sehemu ya huduma
kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Kumbukumbu, Priscilla Moshi (kushoto) na Mkurugenzi wa
Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya (wa pili kulia), wakiwa
na watoto wa Chekechea, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’,
lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya
huduma kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es
Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza kabla ya
kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’ lililokarabatiwa kwa hisani ya
Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya
Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Friday, 16 October 2015
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI AZANIA WAJIFUNZA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ya jijini
Dar-es-Salaam akizima moto kwa kutumia kizimia moto cha aina ya dry
powder baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka
Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Ilala
Wanafunzi wa shule ya Secondari Azania ya jijini
Dar-es-Salaam wakizimamoto kwa kutumia blanketi ya kuzimia moto baada ya
kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala.
WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AFUNGUA MAKTABA YA KOMPYUTA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA LUGOBA MKOANI PWANI
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika sherehe za kukabidhi maktaba ya
Komyuta katika shule ya sekondari ya Lugoba mkoani Pwani
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akifungua maktaba ya kompyuta katika shule ya
sekondari ya Lugoba mkoani Pwani iliyopatikana kwa ufadhili wa Kampuni
ya Mawasiliano ya simu ya Vietnam ya Halotel .Kushoto ni
Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietinam, Nguyen Bac Son na wapili
kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Profesa makame
Mbarawa.
Wednesday, 14 October 2015
RAIS MH.ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MATEMBEZI YA ROTARY DAR MARATHON
RAIS WA AWAMU YA PILI MH.ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MATEMBEZI YA ROTARY DAR MARATHON DAY NA MAKUNDI MBALI MBALI WAKIWEMO WANAFUNZI WA SHULE MBALI MBALI JIJINI DAR ES SALAAM.
Rais wa awamu ya pili Mh.Ali hassan Mwinyi akipunga Bendera ya Taifa kuashiria matembezi ya Rotary Dar Marathon yanaanza.
Mh.Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwa katika mwendo wa taratibu katika matembezi ya Rotart Dar Marathon.
Wanafunzi wa shule za Msingi na Secondary jiji dar es salaam wakiwa katika furaha wakikalibia kumaliza matembezi ya Rotary Dar Marathon.
Wananchi wa makundi mbali mbali wakiwa katika matembezi ya Rotary Dar Marathon.
wanafunzi wakishangilia baada ya kufanikisha kutembea kilomita 5 na wengine 9 katika matembezi ya Rotary Dar Marathon.
Tuesday, 13 October 2015
Watoto wa shule ya awali ya Genesisi wapata mafunzo ya awali ya kuzima moto
Mkaguzi Msaidizi Idd Chanyika wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akielekeza
watoto wa shule ya awali GENESIS jinsi ya kukabiliana na moto wa hatua ya
awali, mafunzo yaliyofanyika katika kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala
jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Msaidizi Idd Chanyika wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka Mkoa
wa Zimamoto Ilala akielekeza watoto kutoka shule ya awali ya GENESIS
waliotembelea kituoni hapo jinsi ya kutumia vazi la
kujikinga na sumu pamoja na bacteria hatari.
Subscribe to:
Posts (Atom)