Watoto wanaotoka familia maskini Longido washindwa kuhudhuria masomo.
Asilimia
kubwa ya watoto wanaotoka katika familia maskini wilayani
Longido mkoani Arusha wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na
changamoto zinazowakabili wazazi wao likiwemo tatizo la njaa,ukosefu
wa huduma ya maji,na Afya.
Wakizungumza wakati wanapokea msaada wa zaidi ya milioni 230
zilizotolewa na mfuko wa Tassaf baadhi ya wananchi wa vijiji
vinavyokabiliwa na matatizo hayo pamoja na kuushukuru mfuko wa
Tasafu wamesema ukosefu wa huduma za kijamii bado ni janga kubwa
kwao na watoto wao.
Baadhi ya viongozi wamesema pamoja na kusisitiza wazazi
kupeleka watoto wao shule wanatembea umbali mrefu na wanapofika
shule wanasinzia badala ya kumsikiliza mwalimu na jambo lililoko
wazi kuwa hawataweza kufanya vizuri.
Wakikabidhi fedha hizo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
longido bw.Felexs Kimario na watendaji wa Tasaff wamesema vijiji
27 vimefikiwa na mpango huo na kaya 259 zimepatiwa msaada huo
ambao ni kwa ajili ya kusaidia elimu afya na kujikimu.
Longido ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Arusha zinazokabiliwa
na tatizo kubwa la ukosefu wa huduma za kijamii ikiwemo
maji,miundombinu ya elimu na Afya.
No comments:
Post a Comment