Thursday, 27 July 2017

SERIKALI YAPIGILIA MSUMARI UDAHILI

 
BAADHI ya vyuo vilivyosimamishwa kufanya udahili katika baadhi ya programu zake, vimebainisha kuwa vimeanza kuchukua hatua ya kuondoa dosari hizo, na viko tayari kufanyiwa uhakiki tena.
Hayo yamebainishwa jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 12 ya Taasisi za Elimu ya Juu nchini yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri, Thadeus Mkamwa alikiri kuwa baadhi ya matawi ya chuo chake, yamesimamishiwa udahili katika baadhi ya programu zake, lakini ni kutokana na tatizo la mawasiliano baina ya chuo hicho na TCU.
“Ni kweli walituletea notisi ya siku 14 tujibu kuhusu upungufu waliobaini, tumewajibu mapema tu, lakini wakati tunasubiria matokeo, tukasikia kwenye vyombo vya habari kuwa, baadhi ya programu zetu zimesimamishwa zisifanyiwe udahili, lakini tunalifanyia kazi,” alisema Mkamwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu nchini. Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Vyuo Vikuu vya Kanisa Katoliki, Atunus Simwambi, alikiri kuwa programu iliyosimamishiwa udahili ilikuwa kwa muda wa miaka mitatu angu ianzishwe haijawahi kuwa na wanafunzi na hivyo kutofundishwa chuoni hapo.
“Programu hii ilianzishwa kwa ajili ya watu wanaotakiwa kuwa mapadri au wanaokwenda kufanya kazi za utume katika maeneo mbalimbali. Kwa kuwa kuna mchakato wa kuunganisha chuo chetu na Chuo cha Filosofia cha Kibosho, tulitarajia programu hii itarejea,” alisema. Chuo hicho kimesitishiwa programu moja ya Bachelor of Arts in Philosophy with Ethics. Naye Makamu wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro (MUM), Profesa Hamza Njozi, pamoja na kukiri kuwa katika baadhi ya programu zilizosimamishwa udahili zilikuwa na changamoto ya walimu, alieleza kuwa dosari hizo zimefanyiwa kazi kama ambavyo Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ilivyoagiza katika notisi yake ya siku 14.
Alisema chuo hicho kilipatiwa notisi ya siku hizo 14 inayoanzia Julai Mosi hadi 14, mwaka huu, kufanyia marekebisho dosari hizo, lakini hata baada ya kutoa majibu, walishtukia kupitia vyombo vya habari, kuwa programu hizo zimesimamishiwa udahili. Akizungumzia taarifa ya TCU, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Watoa Elimu Wasiotegemea Serikali Kusini mwa Jangwa la Sahara(CIEPSSA), Benjamin Nkonya alisema uamuzi huo wa serikali ni nzuri kwani una nia njema ya kurudisha heshima ya elimu nchini.
Nkonya alisema hatua hiyo inapaswa kuungwa mkono na wadau wa elimu nchini kwa sababu yapo baadhi ya mambo ambayo yamechangia kiwango cha elimu kushuka wakiwemo baadhi ya wasomi ambao wameonesha udhaifu kwenye utendaji wao. “Kwanza kabisa tunaona jinsi rais anavyokerwa na baadhi ya wasomi ambao wanavuruga nchi badala ya kuwa kioo, ameona hakuna mwelekeo nah ii inawezekana ikatokana na mfumo wa elimu ambao wakati mwingine baadhi ya shule au vyuo vimetoa elimu isiyokidhi, sasa tunapojisahihisha ni vizuri ili tuwe na mfumo thabiti kwa manufaa ya taifa,” alisema Nkonya.
Alisema kwa bahati nzuri sekta ya elimu nchini kwa sasa imepata mtu sahihi kwenye wizara hiyo inayoongozwa na Profesa Joyce Ndalichako ambaye hata wao wana imani ataendelea kuiboresha zaidi kwa sababu utendaji kazi wake unatambulika. “Profesa Ndalichako ni mtu makini, nakumbuka nilipokuwa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo Vya Serikali (TAMANGSCO) zaidi ya miaka 10, Profesa Ndalichako alipokuwa NECTA, aliadhibu shule au vyuo vilivyokosea, na alitoa adhabu kali hata wakati mwingine kufutia matokeo shule nzima alipobaini udanganyifu, alifanya hivyo kulinda heshima ya elimu,” alisema Nkonya. Hivyo akashauri kuwa uamuzi uliofikiwa na serikali kupitia TCU ni uamuzi sahihi na kuvishauri vyuo husika kufuata maelekezo ili kuhakikisha kiwango cha elimu kitolewacho kina ubora unaotakiwa.

Monday, 17 July 2017

Ulemavu sio mwisho wa kutimiza ndoto, mapacha walioungana watusua kielimu



Maria na Consolata ni wasichana waliozaliwa wakiwa wameungana na sasa wamekuwa na furaha kubwa baada ya kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita.
Mapacha hao wenye umri wa miaka 19 walikuwa wanasoma katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa nchini Tanzania, wamefaulu kwa kupata daraja la pili katika masomo yao ya kidato cha sita na kuwa na matumaini kuwa ndoto yao ya kuwa walimu hapo baadaye inaelekea kutimia.
“Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana,” amesema Consolata.
Baada ya matokeo hayo, Maria na Consolata wamesema kuwa wanapendakuendelea na masomo yao ya elimu ya juu katika chuo kilichopo katika mkoa wanaoishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao wangependa kubadili mazingira, hivyo wamechagua Chuo Kikuu Cha Ruaha.
“Kwanza tunapenda mazingira ya Iringa, hatukutaka kwenda Dar es Salaam kwa sababu ya kwanza tunapenda kuishi pamoja na walezi wetu Masista waliokuwa wanatulea tukiwa wadogo na pili mikoa mingine ni mbali na tunapoishi,” alisema.
Kadhalika, mapacha hao wamesema wamechagua kubakia mkoani kwao kwa sababu ya hali yao, wamesema hawatamudu kuishi kwenye mazingira ya joto. “Mji wa Iringa ni baridi, hali hii tumeizoea.”
Aidha, wametoa wito kwa wazazi, wamesema hakuna linaloshindikana iwapo wazazi watawajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu, wawaone kama watoto wengine na kuwapa mahitaji yao ya msingi, wawawezeshe, wawapatie nafasi ya kujiendeleza maana wakiwezeshwa wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.
” Wazazi washukuru Mungu kupata watoto wenye changamoto kama wao wasione kuwa na mtoto mlemavu ni laana.”

Saturday, 15 July 2017

START UP GRIND DAR HOSTS GODFREY MAGILA

 
Godfrey Magila is the founder and CEO of Magilatech, a software development and security auditing company in Dar es Salaam, Tanzania started in 2012. 
Magilatech launched Tigobackup, a mobile security application performing full content backup on mobile device and antitheft commands. The app has recovered more than 3,600 lost and stolen devices. 
Through his company, Magila employs 14 people, has seven contract employees, made over $1 million last year, has app contracts with Airtel, Vsomo, Maxcom, Selcom and DayOne Softcom. Magila holds a Bachelor of Finance and Accounts degree and is a self-taught programmer. He is also an entree into Forbes Africa 30 Under 30, 2017
 
DON'T MISS IT

POLENI KWA USUMBUFU.....LINK MPYA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2017 IPO HAPA KWENYE BLOG YENU PENDWA KARIBUNI SANA.

 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokoe ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita. 

Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
 
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
Taarifa iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na wavulana ni 35,647.

 Bonyeza HAPA kufatilia matokea ya shule zote Tanzania.
BONYEZA LINK HII HAPA CHINI


Tuesday, 31 January 2017

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

 
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
 
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

==>>Bofya  <<HAPA>  Kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne 2016



Monday, 30 January 2017

MTANZANIA PEKEE AINGIA KWENYE SHINDANO LA DIGITAL PITCH COMPETITION.

 
Julius J. Julius ni Mtanzania Pekee alieingia kwenye mashindano ya DIGITAL PITCH COMPETITION ambayo yantarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini,kijana huyu ndiye anayewakirisha nchi ya Tanzania peke yake.Basi kama Mtanzania unaombwa kumpiga kura kadri uwezavyo ili aweze kuipeprusha Bendera ya Tanzania.
Jinsi ya kupiga kura bonyeza hapa  http://woobox.com/t7kzv8-cpk/gallery/SWEgB8FnaAg
 kisha unakuwa umeshampigia kura huyu kijana waKITANZANIA na unaweza kurudia kupiga baada ya masaa sita tena.Tuonyeshe uzalendo kwa kumsaidia kijana huyu.

Friday, 27 January 2017

ASASI YA HIFADHI YA JAMII KUTOKA IFM (ISPA) YA FANYA DHIARA YA KIMASOMO KWENYE MMAMLAKA YA HIFADHI YA JAMII (SSRA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM.



 Asasi ya Hifadhi ya jamii kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha Ifm,leo hii waitembelea mamlaka ya hifadhi ya jamii,ili kujifunza kwa vitendo jinsi mamlaka hiyo inavyo fanya shughuli zake za kuisimamia secta ya hifadhi ya jamii hapa nchini,wanafunzi hao ni ambao wanasoma fani ya uifadhi wa jamii ambayo inatolewa hapo chuoni kwao.


Makamu wa Rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii ndugu Carolyn Mmari akiongoza wanafunzi wenzake wakati wakujipatia chakula.

  




 Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na furaha baada ya kufika kwenye ofisi za mamlaka ya hifadhi ya jamii leo hii jiji Dar es salaam.


Mkurungenzi wa sharia katika Mamlaka hiyo akiwakaribisha wanafunzi hao kwa niaba ya Mkurungenzi mkuu.


 
 


 
Mmoja ya wanafunzi pamoja na afisa wa mmalaka ya hifadhi ya jamii wa kifatilia kwa umakini semina ikitolewa na afisa wa mamlaka ya fidhai ya jamii.
 

 Rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii Bwana Sylvester Dionizy kutoka chuo cha usimamizi wa Fedha IFM,akitoa neno la shukrani kwa Mamlaka kupokea wito wao wakuja kujifunza hapo ofisi kwao.


 Afisa wa Mamlaka ya hifadhi ya jamii akishukuru ushiriki wawanafunzi kutoka chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) na kutambua umuhimu wa watalam wa Hifadhi ya Jamii Katika Nchi yetu.
 
 

 Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Asasi ya Hifadhi ya Jamii na maafisa wa mamlaka ya Hifadhi ya jamii.