Friday, 22 July 2016

WANAFUNZI WA SUA WALITOKA SJUIT WAPIGA KAMBI BODI YA MIKOPO.




Na Asnain Chionda JR.



 
Wanafunzi wanaosoma katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) Waliohamishiwa na Serikali chuon hapo wakitokea chuo kikuu cha mtakatifu Joseph tawi la Songea,  Leo wamepiga kambi katika bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (Heslb) wakishinikiza bodi hiyo kuwalipa pesa zao za kujikimu walizocheleweshewa kwa kipindi cha Miezi minne. 
Wanafunzi hao ambao wanasoma chuon hapo wameshindwa kuendelea kuvumilia kukaa chuoni hapo kwa ahadi za kila siku kutoka bodi hiyo.
Aidha, wanafunzi hao ambao wameamua kupanda basi kutoka Chuon kwao Morogoro had Dar es salaam zilipo ofisi hizo, wamesikitishwa na kitendo cha bodi ya mikopo kutokuwajali na kushughulikia matatizo ya wanafunzi hao kwa muda huo wote tangu walipowasili chuoni hapo mapema mwezi wa Tatu mwaka huu hali iliyowalazimu wanafunzi hao kupiga kambi ofisini hapo.
Hadi kufikia muda ambao taarifa hizi zinapelekwa kwenye mitambo ya Scholars Blog,  wanafunzi hao bado wapo katika ofisi za bodi hiyo wakisubiri mrejesho kutoka kwa mtendaji mkuu wa bodi anaehusika na utoaji wa pesa hizo kwa wanafunzi ambae ameahidi kushughulikia Suala hilo haraka iwezekanavyo.


 
 
 
 
 
 








Afisa wa Bodi ya Mikopo akitoa maelekezo kwa wanafunzia hao.



Sunday, 17 July 2016

TCU YATOA UFAFANUZI JUU YA UDAILI WA WANAFUNZI KWENDA VYUO VIKUU.

Tume ya vyuo vikuu (TCU) imetoa ufafanuzi kuhusu alama zitakazowezesha mwanafunzi kudahiliwa Chuo Kikuu baada ya kuchanganya wengi.

Yasema inatakiwa mwanafunzi awe na principal pass mbili walau zifikie point 4 kwenye masomo mawili na si lazima ziwe D mbili.


Monday, 11 July 2016

WAZIRI ATEMBELEA BANDA LA PSPF


Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Angelina Mabula, (kulia), akimsikilzia AfisaMasoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mgire Werema, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwnye viwanja vya Mawlimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia Mpango wa PSS, Fatuma C. Luwago, kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,

 Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania, (TANTRADE), Theresa H. Chilambo, (kushoto), akijaza fomu za kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa hiari kwenye banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa , Dar es Salaam, Julai 8, 2016. Anayemuhudumia ni Joseph Lyimo, kutoka kitengo cha Mawasiliano PSPF.


Afisa Huduma kwa wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Judith Mtweve, (kushoto), akimuhudumia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 8, 2016



 Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye banda la Mfuko huo wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 8, 2016,

YOUTH AWAKENING FOR CULTURAL AND WILDLIFE TOURISM DEVELOPMENT ORGANIZATION (YACWDO) YA ST.AUGUSTINE MWANZA



YOUTH AWAKENING FOR CULTURAL AND WILDLIFE TOURISM DEVELOPMENT ORGANIZATION (YACWDO) iliopo chini ya wanafunzi wa mwaka wa pili tourism(UTALII) SAUT- MWANZA watembelea kivutio cha asili BUJORA MUSEUMS kilichopo kisesa


JOHN LWEGANWA ambaye ndio Mwenyekiti YACWDO akiwa katika pozi la picha hapo kwenye kituo cha utali.


Mwenyekiti msaidizi Bw. GEORGE W. LEMA  akiwa kwenye ngazi za kuelekea kwnye nyumba ya mfalme wa kisukuma.



Katibu wa YACWDO akiwa katika pozi maridadi


 John Valerian, Uagai usiri, Raymond Kisasembe na Mwenyekitiki Msaidizi George W. Lema kwenye chumba cha ngoma zenye miaka 500 cha mfalme wa kisukuma.


 John Kayanda, Hagai Usiri na Naomi Nkya katika selfie.


 Benitto Mosha, Kachenje Mzirai, Marco Evarist, Hagai Usiri, Raymond Kisasembe, George W. Lema, Daniel Yowas na wengne katika picha ya pamoja.


 Members wa YACWDO katika picha na nyoka waliopo BUJORA.

 Members waYACWDO kwenye picha ya pamoja.


Imeripotiwa na George W.Lema kutoka St.Augustine Mwanza.

BENKI YA NBC YAZINDUA PROGRAM YA WAJIBIKA KUSAIDIA AJIRA KWA VIJANA WANAOHITIMU VYUO NA TAASISI YA ELIMU YA JUU.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (wa pili kulia), na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), James Kinyanyi (wa pili kushoto), wakibonyeza kitufe cha kompyuta kuashiria uzinduzi wa program ya Wajibika ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kushoto ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo na Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde, akishiakana mikono na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Neema Rose-Singo (kushoto), baada ya kuzindua program ya Wajibika ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wapili kushoto ni; Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, James Kinyanyi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi.




Mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program ya Wajibika ya benki hiyo yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni; Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC,James Kinyanyi, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (kulia), akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa program ya Wajibika ya Benki ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi katika hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe akizungumza katika hafla hiyo katika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mlimani jijini Dar es Salaam juzi



Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde (katikati), akiongozana na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe(kushoto), na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Prof. Cuthbert Kimambo (kulia), wakati akiingia katika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam juzi kuzindua program ya Wajibika ya Benki ya NBC yenye lengo la kuwandaa vijana wahitimu wa vyuo na taasisi za elimu ya juu kuingia soko la ajira rasmi na binafsi.




Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na washiriki wengine waliohudhuria uzinduzi huo wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.




Mgeni rasmi katika uzinduzi wa program ya Wajibika ya Benki ya NBC, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (katikati),akipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na maofisa wa NBC ambao kwa namna moja ama nyingine wamefanikisha uzinduzi huo.

Saturday, 9 July 2016

PICHA YA SIKU




Maandiko yanasema usimwache elimu aende zake!jitihada na kujituma zitafanikisha malego yako.
Picha kwa hisani ya Mtaa Kwa Mtaa blog

Friday, 8 July 2016

'ELIMU NI MUHIMILI WA TAIFA', UNGANA NA CAMPUS VYBEZ NDANI YA PROTEA HOTEL JULAI 9, 2016


Ili kupambana na changamoto za ajira Nchini kama kijana hususani mwanafunzi wa elimu ya juu, unaitaji mbinu mbadala za kujikwamua kimaisha. #CampusVybez ya #TimeFm @timesfmtz @sandytemu @djj_one @ inakukutanisha wewe kijana na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi ajira na vijana Antony Mavunde, kuzungumzia mbinu za kujikwamua kwenye ajira @anthonymavunde Jumamosi hii Protea Hotel, saa mbili kamili asubuhi.

Friday, 1 July 2016

TUNAPENDA KESHO KUWA KARIBISHA KWENYE UZINDUZI WA BLOG YETU YA KISWAHILI



Uzinduzi utafanyika kwenye kipindi cha #elimikawikiendi kwenye mtaandao wa twitter hapo kesho kuanzia sa mbili asubuhi!mnakaribishwa wote,wafate kwenye twitter @EW_Tanzania   na @sdionizy