Thursday, 4 February 2016

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu aongoza kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi

 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Leornad Akwilapo akiongea na washiriki (hawapo pichani) wa kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) kinachofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara Mkoani Tanga. 

 
 Mwakilishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania, Silyvia Lupembe akiwa elezea washiriki wa kikao kazi cha upitiaji na uboreshaji wa miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) jinsi Mamlaka hiyo ilivyojipanga katika kuhakikisha inafadhili mafunzo ya walimu ili kuboresha elimu nchini.

 
 Mmoja wa washiriki wa kikao kazi cha upitiaji na uboreshaji wa miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) akitoa maelezo ya jinsi wanavyofanya kazi hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt Leonard Akwilapo.
 
 
Washiriki wa kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Leornad Akwilapo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho katika Shule ya Sekondari Usagara Mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment