Sunday, 21 February 2016

TPB YAKABIDHI SHULE VYOO VYA THAMANI YA TSH.MILIONI 4.7

 Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14, vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa 
Wanafuzni wakishangilia kupata vyoo
 
 Sehemuya vyoo hivyo

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Makambi iliyopo Kata ya NdilimaLitembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania. 

BENKI ya posta Tanzania, TPB, imekabidhi vyoo vyenye thamani ya shilingi milioni 4.7 kwa shule ya msingi Makambi iliyoko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Akikabidhi vyoo hivyo vyenye matundu 14 vilivyojengwa na benki hiyo ili kusaidia kuondokana na upungufu wa vyoo kwenye shule hiyo mwishoni mwa wiki, Meneja mahusiano na mawasiliano wa TPB, Noves Moses, alisema msaada huu wa benki nisehemu ya mchango kwa jamii katika kuboresha miundombinu ya shule na hivyo kufikia lengo la kutoa elimu bora hapa nchini.
Kwa kutambua juhudi za Rais za kutoa elimu bure kwa wanafunzi kote nchini, ambapo kumekuwepo na ongezeko kubwa sana la wanafunzi, benki ya posta inayofuraha kuunga mkono juhudi za Mh.Rais na msaada huu wa vyoo utasaidia kuweka mazingira bora ya utoaji elimu lakini pia mahudhurio ya wanafunzi, alisema Noves.
Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wadau wa elimu kulichukulia suala la elimu bure kama kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake wanadai ni kazi ya serikali pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji elimu.
 
“Suala la elimu bure lisiwe kigezo cha wadau kushindwa kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha” alisemaMeneja huyo wa mahusiano na mawasiliano.
Noves alisema kuwa Benki ya Posta Tanzania inafanya kazi kwa kiwango kikubwa na serikali hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na elimu huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Kanisius Ngongi awali akitoa taarifa ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa vyoo hivyo alisema kuwa shule hiyo inawanafunzi 850 na matundu ya vyoo yapo 14 na kuwa vyoo vyote vina maji ya kutosha.
Ngongi aliipongeza benki hiyo alisema kuwa shule hiyo kwa sasa imeshabadilika,mazingira yamekuwa bora kwa upande wa vyoo vya wanafunzi ambavyo kwa sasa hakuna shule ndani ya Manispaa hiyo yenye vyoo kama hivyo.
Mwalimu Ngongi alisema kuwa licha ya vyoo vya wanafunzi kuwa bora lakini bado kunachangamoto ya vyoo vya walimu maana vyoo walivyokuwa wakivitumia vimeshapoteza ubora wake na kuwafanya walimu hao kupata shida mahala pa kujisitili hivyo amewaomba wadau mbalimbali waweze kuchangia kama Benki ya Postainavyojitolea.

 

Saturday, 6 February 2016

MABALOZI WA PSPF PAMOJA NA MC RUVANDA WATOA SOMO KUHUSU ELIMU YA AJIRA (THINK BEYOND EMPLOYEMENT)

Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) Bw.Ahadi Kitaponda akifungua semina iliyopewa jina la Think Beyond Employment iliyofanyika hapo chuo kikuu cha Dar es salaam. 
Wanafunzi wa vyuo mbali mbali vya jijini Dar es salaam wakifitatilia semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Afisa mwendesheji wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF akitoa elimu kwa wanazuoni walioshiriki katika semina hiyo.

Mmoja wa wanazuoni akiluliza swali kwa afisa mwendeshaji wa PSPF.

 
 
Balozi wa mfuko wa PSPF Mrisho Mpoto akitoa darasa kwa wanazuoni
 
 
Baadhi ya wanazuoni wakifatilia maada kwa umakini.

 
Balozi wa PSPF Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wanazuoni walioshiriki kaktika chuo kikuu cha Dar es salaam.
 
Wanazuoni hao wakifuatilia kwa makini.
 
 
Afisa muendeshaji wa mfuko wa hiyali akitoa darasa kwa wanazuoni kaktika chuo kikuu cha dar es salaam.
 
 
Mc Ruvanda akitoa elimu juu ya swala la ajira nchini hapa.
 
 
Balozi wa PSPF na mwana mitindo wakimataifa Flaviana Mtata akitoa historia fupi ya maisha yake na kuwasii vijana kijituma na kutumia fursa vizuri.
 
 
Wanazuoni wakifuatilia kwa makini mwana mitindo Flaviana Matata wakati akizungumza
 

 
Wanafunzi akielekezwa na afisa wa mfuko wa hiyali wa PSPF jinsi ya kujiunga mfuko huo.
 

 
Baadhi ya wanafunzi wakijiunga kwenye mfuko wa hiyari wa PSPF.
 
 
Mezaa kuu ikifuatilia mjadala kwa makini.
 
 
Wanafunzi wakipiga kura kumsaaidia balozi wa PSPF Mrisho Mpoto aliyechaguliwa katika mashindano ya Kora Africa.
 
 
Afisa wa uendeshaji wa PSPF akitoa darasa kwa mwanazuoni jinsi mfuko unavyo fanya kazi zake.
 
 
Afisa makoso wa PSPF Bi.Rahma akimsaidia Rais wa Daruso kujiunga na mfuko wa hiyali ya PSPF.
 
 
Mc Ruvanda akijadiliana na Makumu wa Rais wa Daruso wakati wa kujaza fomu ya uanachama wa mfuko wa hiyali.
 
 
 
Wanafunzi wakipiga picha ya pamoja arimaarufu kama (selfie) na wageni ramsi.
 
 

 
Picha ya pamoja wa maafisa wa PSPF,mabalozi wa PSPF,Mc Ruvanda na serikali kuu ya wanafunzi DARUSO.


Thursday, 4 February 2016

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu aongoza kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi

 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Leornad Akwilapo akiongea na washiriki (hawapo pichani) wa kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) kinachofanyika katika Shule ya Sekondari Usagara Mkoani Tanga. 

 
 Mwakilishi wa Taasisi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania, Silyvia Lupembe akiwa elezea washiriki wa kikao kazi cha upitiaji na uboreshaji wa miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) jinsi Mamlaka hiyo ilivyojipanga katika kuhakikisha inafadhili mafunzo ya walimu ili kuboresha elimu nchini.

 
 Mmoja wa washiriki wa kikao kazi cha upitiaji na uboreshaji wa miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) akitoa maelezo ya jinsi wanavyofanya kazi hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt Leonard Akwilapo.
 
 
Washiriki wa kikao kazi kwa ajili ya kuboresha miongozo ya Programu ya Kujenga Uwezo wa Walimu na Wanafunzi –Student Teacher Enrichment Programme (STEP) wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Leornad Akwilapo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho katika Shule ya Sekondari Usagara Mkoani Tanga.