Monday, 18 January 2016

BONNAH EDUCATION TRUST FUND WAZINDUA KAMPENI YA ‘MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA

 
 Mwanamitido wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana.


 Wageni waalikwa kutoka Jimbo la Segerea wakiwepo wananchi wa kawaida wakifuatilia tukio la uzinduzi wa kampeni hiyo.

Mbunge wa Segerea Mh.Bonnah Kaluwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment