Saturday, 30 January 2016

PSPF YASAIDIA VITI KITUO CHA WALIMU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

  Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, (kushoto), na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Scola Mnyamani, wakiwasili kwenye kituo cha Walimu Mbagala jijini Dar es Salaam, Januari 29, 2016
 
  Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, na Afisa Masoko na Mahusiano wa Mfuko huo, wakiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbagala.
 
 Bw. Mselem akiteta jambo na balozi Mpoto.
 
 
  Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Francis Mselem, (kulia), akipeana mikono na baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye kituo hicho wakati akiwakabidhi viti.
 
 Bw. Mselem akitoa hotuba. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Mkuu wa kituo hicho, Fausta Lugola.
 
 Balozi Mpoto, akitoa darasa kuhusu huduma za Mfuko huo.
 
  Meneja Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Francis Mselem, (kulia), akipeana mikono na baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye kituo hicho wakati akiwakabidhi viti.
 
 Bw. Mselem akipena miko na mwakilishi wa Afisa Elimu Manispaa ya Temeke, Bw.Adolph Shayo.

FLAVIANA MATATA NA MO DEWJI FOUNDATION WAKABIDHI MSAADA WA CHOO SHULE YA MSINGI MSINUNE, BAGAMOYO



Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Pwani. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto (kulia). Katikati ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto (kulia) alipowasili kwenye hafla fupi ya kukabidhi choo kilichojengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.


Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation, Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakiwa pamoja na baadhi ya watu walioongozana nao wakielekea kwenye eneo la tukio.
Muonekano wa jengo la choo ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.

Muonekano wa choo ambacho kilikuwa kikitumika awali kabla ya ujenzi wa choo kipya ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa Mo Dewji Foundation.




Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi kwa pamoja wakifunua kitamba kuzindua jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa vyoo vya kisasa katika Shule ya Msingi Msinune Bagamoyo



Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akikata utepe kuzindua rasmi choo cha kisasa katika shule ya Msingi Msinune kilichojengwa na Mo Dewji Foundation. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakishuhudia tukio hilo.

Taasisi ya Mo Dewji ikishirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata, imekabidhi choo katika Shule ya Msingi Msinune ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani kitakachosaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Tukio la kukabidhi choo hicho limefanyika katika shule hiyo mapema leo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana Matata ambapo ameelezea kuwa, wamekua wakiwapatia wanafunzi wa Msinune vifaa vya shuleni tangu mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka jana aliombwa kuwa mlezi wa Shule na kuweza kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo suala hilo la vyoo vya waalimu na wanafunzi, madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Flaviana amesema baada ya kuguswa aliweza kumshirikisha Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji, alikubali kutoa msaada huo kupitia taasisi yake hiyo ya Mo Dewji Foundation na kuweza kujenga choo hicho chenye matundu nane.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo ya Msinune, Bw. Msami Mgoto ameshukuru taasisi ya Mo Dewji kwa msaada wa kufadhili ujenzi wa choo hicho huku akielezea kuwa itasaidia wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma hapo licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhani Mtokeni aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Msinune huku akiomba iendelea kuwasaidia pindi wanapokuwa na matatizo.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi amepongeza juhudi za Flaviana Matata za kusaidia jamii ikiwemo kukua kwa elimu hapa nchini hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Francesca ameongeza kuwa, Mo Dewji kupitia msaada huo, wanafunzi watakuwa katika mazingira mazuri na safi kwa afya zao ikiwemo kusoma bila kuwa na tatizo la awali la choo, kwa sasa na miaka ijayo choo hicho kitakuwa mkombozi na msaada mkubwa.

Tuesday, 26 January 2016

CHANGAMKIA FURSA MUHIMU KWENU VIJANA SHINDANO LENYE FURSA YA KUKUZA MITAJI KWA VIJANA LA MO MJASIRIAMALI LAZINDULIWA

Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji
 
Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited leo (jumatatu) wamezindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasiriamali miongoni mwa vijana.
Shindano ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali Tanzania.
“Mimi kama Mjasiriamali kijana na mzaliwa wa Singida vijijini, sikufikiria hata mara moja kama leo ningekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa moja ya makampuni yaliyofanikiwa sana katika nchi yetu na hata barani Afrika.” Inasema taarifa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MeTL kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.
Aidha alisema Afrika ni moja ya bara linalokua kwa haraka na lenye ukuaji imara wa uchumi na amini vijana wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kutumia fursa hizo ili kujiletea uchumi endelevu.
Lakini pamoja na ukweli huo changamoto kama za ukosefu wa mitaji, ukuzaji ujasiriamali na mitandao ya biashara zimekatisha tamaa vijana wengi kukuza kwa mafanikio makampuni yao hapa Tanzania na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa watu wa kipato cha kati.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), watu wenye kipato cha kati katika bara la Afrika wataongezeka na kufikia watu bilioni 1.1 ifikapo mwaka 2060.
Watu wa kipato cha kati ndio wanaochagiza ukuaji wa uchumi kutokana na mahitaji yao na pia ari ya ujasirimali.
Pamoja na ukweli huo kunachangamoto nyingi zinawakabili watu hao wa kipato cha kati. Mathalani nchini Tanzania changamoto kubwa kwa vijana wajasirimali ni gharama za kutafuta mtaji kwa kazi hizo.
“Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba vijana hawa wanaondolewa tatizo la ujasirimali ili waweze kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.” inafafanua taarifa hiyo.
Aidha kwa kuwa Tanzania inaelezwa kuwa ni nchi ya 19 katika bara la Afrika kuhusiana na fursa na ujasirimali ipo haja ya kusaidia ili kuiondoa katika nafasi hiyo. Taarifa ya nafasi ya Tanzania imo katika ripoti yake ya mwaka 2014 ya Africa Prosperity Report.
Taarifa ilifafanua zaidi kwamba kutokana na haja hiyo Taasisi ya Mo Dewji na Darecha Limited wameungana pamoja na kuanzisha shindano la Mo Entrepreneurs ili kutambua na kuuenzi mchango wa wajasirimali chipukizi na kufanikisha ndoto zao.
Ili kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL Group na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation) ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na kuikuza.
Mambo hayo yatatekelezwa katika mfumo wa shindano litakalogusa wajasiriamali ambao wana ari na nia ya dhati ya kuendeleza shughuli walizofikiria na kuzianzisha kwa lengo la kuinua uchumi wao binafsi na wa taifa.
Washindi watatu watakaotangazwa Aprili mwaka huu watapatiwa mtaji wa kuanzia au kuendeleza, pia watapatiwa maarifa ya kuendeleza shughuli zao na kuanzishwa mtandao wa kibiashara na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL Group na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji.
Wakati akipewa tuzo ya Forbes ya mwaka 2015, Mohammed Dewji aliitoa kwa heshima ya vijana akiwatakia kila la heri waking’aa, kuvunja nira ya woga, kukabili changamoto na kuendelea katika ujasiriamali kwa lengo la kufanya dunia yetu mahali bora pa kuishi.
 
 kupata fomu ya maelezo naya kushiriki bonyeza hapa http://www.modewjifoundation.org/mo-entrepreneurs-competition
 

Monday, 18 January 2016

BONNAH EDUCATION TRUST FUND WAZINDUA KAMPENI YA ‘MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA

 
 Mwanamitido wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana.


 Wageni waalikwa kutoka Jimbo la Segerea wakiwepo wananchi wa kawaida wakifuatilia tukio la uzinduzi wa kampeni hiyo.

Mbunge wa Segerea Mh.Bonnah Kaluwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.

Sunday, 17 January 2016

PEPSI NA MAGIC FM ZA DHAMINI KIKAMILIRIFU ASASI YA HIFADHI YA JAMII YA IFM (ISPA) KWENYE MAANDAMANO YA AMANI NA BONANZA LA MICHEZO DHIDI YA UPINGAJI MAUWAJI NA UNYANYASAJI ZIDI YA WATU WENYE UALBINO

 
Wanafunzi wa Asasi ya Hifadhi ya Jamii wa IFM (ISPA) wakijianda kwa kuanza ramsi maandamano ya Amani ya kupinga mauwaji na unyanyasai ya watu wenye ualbino
 
 

 
 
 
 
 
 Wakiwa katika maandamano na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti dhidi ya kupinga hukatili ya watu wenye ualbino.
 Mkuu wa kitivo cha Bima na Hifadhi ya jamii wa IFM Dr.Abdallah Saqware akiwa kwenye maandamano pamoja na wanafunzi wake.
 
 
 
Wananchi mbali mbali jiji dar es salaam wakitazama maandamano ya wanafunxi wa chuo cha usimamizi wa fedha.
 
 
 
 
 Jeshi la polisi nalo halikuwa nyuma katika swala la ulizi katika maandamano ya wanafunzi wa Asasi ya Hifadhi ya jamii (ISPA).
 
 
 Wageni ramsi wakifuatlia hutuba mbali mbali wakiongzwa na rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii (ISPA) Bw.Innocent Kembo aliyeshika shavu.
 
 
 
 
 
 
Bw.David alimarufu Ecrow akisoma taarifa ya habari.
 
 Rais wa Asasi ya Hifadhi ya Jaminii bw.Innocent Kembo hakizungumza na halaiki ya watu walio kuja kwenye bonanza hilo.
 
 
 
 Mwenyekiti wa Asasi ya Bima na Majanga katika chuo cha usimamizi wa fedha akizumza machache juu ya bonanza hilo. 
 
 
 
Waziri wa habari Nape Nnauye akipata maelekezo juu ya mafuta ya sun cream ambayo hutumika kuzuia mionzi ya jua kwenye ngozi za watu wenye ualbino.
 
 Waziri wa habari Nape Nnauye akiteta kidogo na Rais wa Asasi wa Hifadhi ya jamii bw.Innocent Kembo
 
 
 Washiri wamakundi mbali mbali walikuwepo ikiwemo pamoja na SYDS
 Picha ya pamoja ya timu ya Amani na Upendo kabla ya mpira kuanza kuonyesha kuwa watu wenye ualbino kuwa nao wanaweza kila kitu kama sisi ambao hatuna ualbino.
 kikosi cha timu ya Amani katika picha ya pamoja
 Kikosi cha timu ya Upendo kaitika picha ya Pamoja
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 Picha mbali mbali katika michezo tofauti tofauti katika bonanza hilo.
 
 Bwana Josephat Tona akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Asasi ya Hifadhi ya jamii.
 
 Rais wa Asasi ya Hifadhi ya jamii Bw.Innocent Kembo akiongea na Mkuu wa Idara ya Bima na Hifadhi ya jamii Dr.Abdallah Saqware kaitika Bonanza hilo.
 
 
 
 
 Picha mbali mbali za watu wakifuatilia Bonanza kwa umakini.
 
.
 
 
 
 

Bwana Josephat Toner akitoa neno la kushukuru kwa niaba ya watu wenye Ualibino katika bonanza hilo.