Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua
kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana
simu bure.
Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi
hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha
na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi
wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.
Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia
huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou
vyao, ujumbe huo ulisema.
Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa,
Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack,
kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza
kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.
Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na
Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music,
Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja
wa Tigo kuweza kurudisha simu na
zinapoibiwa au kupotea.
Kujisajili
kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba
ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka
Tigo.
Meneja
Mauzo wa mkoa wa Tanga kutoka Tigo Bw.Daniel Mainoya akiongea na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali , kuhusu uzinduzi wa
kifurushi kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo katika Uwanja
wa chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, mjini Tanga.
Mwanafunzi
kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella
Mwakiliku akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
Mwanafunzi
kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, Bw.Albert Risala akiongea na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi
wamekipokea kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka
Tigo.
Kikundi
cha sarakasi kikitumbuiza wanafunzi katika uzinduzi wa kifurushi cha
University pack kilichoboreshwa katika uwanja wa chuo cha Utumishi wa
Umma,Kange, mjini Tanga.
Msanii
wa kizazi kipya Roma Mkatoliki akiwatumbuiza wanafunzi wa chuo cha
Utumishi wa Umma,Kange, mjini Tanga,katika uzinduzi wa kifurushi cha
University pack kutoka Tigo kilichoboreshwa.
No comments:
Post a Comment