Tuesday, 17 November 2015
WANAFUNZI WA VYUO KUFURAHIA HUDUMA YA KUPIGIANA SIMU BURE
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imezindua
kifurushi maalum kinacho wawezesha wanafunzi, ambao ni wateja wa Tigo, kuweza kupigiana
simu bure.
Huduma hii imeboreshwa zaidi baada ya kifurushi
hicho kwa jina maarufu kama Tigo Uni Pack kuzinduliwa mwaka jana, ukilinganisha
na kifurushi cha zamani, kifurushi hichi kipya cha wiki kitawapatia wanafunzi
wepesi wa kujiunga wakiwa popote ndani ya nchi, hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya Tigo leo.
Kinachohitajika ili wanafunzi waweze kutumia
huduma hii,ni kuhakiki kwamba wamesajiliwa kama wateja wa Tigo katika Vyou
vyao, ujumbe huo ulisema.
Akizungumzia kifurushi hicho kilichoboreshwa,
Meneja wa Bidhaa kutoka Tigo Edwin Mgoa,alisema kifurushi hicho cha Uni Pack,
kinadhirisha vipi Tigo inavyowasaidia wanafunzi kwa ajili ya kuwawezesha kuweza
kupata huduma za mtandao za maisha ya kidijitali.
Baadhi ya huduma za kidijitali zinazotelewa na
Tigo ni upatikanaji wa muziki bila kikomo kwa kupitia huduma ya Tigo Music,
Facebook ya Kiswahili, Tigo Pesa App, Tigo Backup- huduma inayowawezesha wateja
wa Tigo kuweza kurudisha simu na
zinapoibiwa au kupotea.
Kujisajili
kwa kifurushi cha Uni Pack, mwanafunzi atahitajika kupiga *148*01*20#, namba
ambazo kwa mujibu wa taarifa hiyo, imejumuisha vifurushi vingine muruwa kutoka
Tigo.
Meneja
Mauzo wa mkoa wa Tanga kutoka Tigo Bw.Daniel Mainoya akiongea na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali , kuhusu uzinduzi wa
kifurushi kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo katika Uwanja
wa chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, mjini Tanga.
Mwanafunzi
kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange,mjini Tanga, Bi.Stella
Mwakiliku akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi wamekikubali kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka Tigo.
Mwanafunzi
kutoka chuo cha Utumishi wa Umma, Kange, Bw.Albert Risala akiongea na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu vipi wanafunzi
wamekipokea kifurushi hicho kilichoboreshwa cha University Pack kutoka
Tigo.
Kikundi
cha sarakasi kikitumbuiza wanafunzi katika uzinduzi wa kifurushi cha
University pack kilichoboreshwa katika uwanja wa chuo cha Utumishi wa
Umma,Kange, mjini Tanga.
Msanii
wa kizazi kipya Roma Mkatoliki akiwatumbuiza wanafunzi wa chuo cha
Utumishi wa Umma,Kange, mjini Tanga,katika uzinduzi wa kifurushi cha
University pack kutoka Tigo kilichoboreshwa.
Saturday, 14 November 2015
PSPF,NSSF,GEPF NA TIGO WAZAMINI BONANZA LA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)
Mkuu wa chuo cha Usimamizi wa Fedha Prof.Godwin Mjema ( mwenye tisheti ya blue) akiwa na waandalizi wa bonanza la wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM).
Rais wa wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) bwana Eliaza akitoa maelekezo kabla ya bonanza kuanza rasmi.
Mwalimu wa malezi kwa wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha akitoa maelezo na jinsi ya kufata sheria katika bonanza hilo.
Mkuu wa chuo cha Usimamizi wa fedha akiwasalimu wanafunzi na kuwa shauri kufanya mazoezi kila wakati na kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo.
Mkuu wa chuo cha Usimamizi wa fedha Prof.Godwin Mjema akiweka mpira sawa kabla ya kuzindua bonanza rasmi.
Mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha Prof.Godwin Mjema akipiga shuti kuashiria bonanza limeanza rasmi.
Timu wa wafanzakazi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha wakiwa katika picha ya pamoja kabla bonanza kuanza ramsi.
Timu ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa fedha wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya
bonanza kuanza.
Waziri wa michezo bwana Mkami akipeana mkono na mkuu wa chuo cha IFM wakati wakukagua vikosi vya wachezaji.
bonanza kuanza.
Waziri wa michezo bwana Mkami akipeana mkono na mkuu wa chuo cha IFM wakati wakukagua vikosi vya wachezaji.
Wakiwa katika kupeana ushauri kama ilivyo desturi kabla ya mpira kuanza.
Makamu wa rais wa selikali ya wanafunzi wa chuo wa usimamzi wa fedha akiwa uwanjani.
Mwalimu wa michezo bwana Mula Mula akipiga penati ya ushindi na kuweza kuwa washindi dhidi ya wanafunzi wa serikali ya wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha wakifuatilia michezo mbalimbali kwenye bonaza hilo.
Walimu nao awakuwa nyuma kwenye ufuatiliaji wa michezo mbali mbali katika bonanza hilo.
Timu za mpira wa kikapu zikipeana ushauri kabla ya mchezo huo kuanza.
Wanafunzi akijitaidi kufunga goli katika mchuano huo.
Wakina dada nao hawakuwa nyuma,wakiwa katika mazoezi ya mwanzo kabla kuanza kucheza.
Baadhi ya walimu wakitoka uwajani baada ya kumaliza papmabano na kuwa washindi dhidi ya selikali ya wanafunzi.
Maafisa wa mfuko wa Penshensi wa PSPF wakiwa katika banda lao.
Afisa uhusiano mwandamizi bwana Abdul Njaidi akimsajirisha Rais wa chuo cha usimamizi wa fedha katika mpango wa kuchangia kwa hiyali.
Maofisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa juu wa serikali ya wanafunzi baada ya kujiunga na mpango wa kuchangia kwa iyali.
Thursday, 12 November 2015
MWANAFUNZI IFM SOCIAL PROTECTION ALUMIN ESTERSIA NGOWI ATOA MSAADA KWENYE HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Estersia Ngowi mwenye surualii ya bluu akiwa pamoja na marafki zake walio
kuja kutoa msaada pamoja naye kwenye hospitali ya mwananyamala.
Wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vifaa walivyo kuja kukabidhi hospitalini hapo.
Nesi wa zamu alikuwa hakiwa anawapamaelekezo na shida mbali mbali wanazo zipata wangojwa hasa wakina mama katika wodi ya watoto wachanga.
Wakiwa wanakabidhi baadhi ya vifaa walivyokuja navyo kwa Nesi ya zamu katika wodi wa watoto wa changa.
Wakiwa wanaelekea wodini kutoa na kukabidhi baadhi ya vifaa waivyo kuja navyo.
Friday, 6 November 2015
HESLB yajivua lawama wanafunzi vyuo vikuu kukosa mikopo 2015/2016
Zaidi
ya wanafundi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu
kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu (HESLB).
Hayo
yamebainika ikiwa ni siku nne tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi
waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi
kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.
Katika
mwaka huu wa masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi
12,000 pekee sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya
idadi ya wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji
wote.
Wanafunzi
waliokosa mikopo ya kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na hivyo
wazazi wao kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa na
hali hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee kwani
hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiliwa na serikali.
Wanafunzi
hao walionekana kukata tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga na elimu
ya chuo kikuu, wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku wakiongozana na
baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.
“Nimetokea
Tabora, wazazi wangu walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa
mikopo na serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu,
nimebakiwa na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu
hatustahili kuteseka hivi,” ameeleza Abdul Omary mwanafunzi mteule UDSM.
Fatuma
Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM, amesema: “Siwezi kujiunga na
Chuo bila mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo itusaidie
hatuna tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze kupata
mikopo na kuanza masomo.”
Waziri
wa Mikopo serikali ya wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza
kutokukubaliana na majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo
kwani yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini kusoma
chuo kikuu.
“Hapa
UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata mikopo kati ya wanafunzi 7,000
waliopangiwa kuanza masomo, hili ni janga kubwa kwa watoto wa masikini
kwani hawawezi kujisajili chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka
walipe ada na wengi wametoka mikoani.
“Tunachukua
hatua moja mbele na kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa
wizara ya elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado
wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi
wanateseka” ameeleza Shitindi.
Mkurugenzi
wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amewaambia
wanahabari waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili kulaumiwa kwani
serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio yenye uwezo wa
kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati husika
Subscribe to:
Posts (Atom)