UTORO MASHULENI KWA WATOTO WA KIKE WAPUNGUA MKOANI MTWARA
Baadhi
ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Chuno ya Mkoani
Mtwara,wakiendelea na masomo yao baada ya kunufaika na mradi wa”Hakuna
wasichoweza”unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wakati wa
hedhi ili waendelee na masomo yao mashuleni.Mradi huo umedhaminiwa na
Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
TATIZO
la watoto wa kike mkoani Mtwara kukatiza masomo kutokana na sababu
mbalimbali limepungua kwa kiasi kikubwa baada ya uwepo wa mradi wa
“Hakuna wasichoweza” unaoendeshwa na T-Marc kwa ufadhili wa Vodacom
Foundation.
Mradi
huo umeonyesha mwelekeo wa kuweza kutatua matatizo yanayowakabili
watoto wa kike kutotimiza wajibu wao wa masomo mashuleni, ikiwa ni
pamoja na kutotimiza ndoto zao sambamba na kupunguza utoro.
Akizungumza
wakati wakati wa mrejesho wa mwenendo wa mradi huo kwa wadau wa elimu
wa mkoa huu, Meneja wa Mradi huo, Doris Chalambo alisema mradi huo
ulioanza kutekelezwa mwaka 2013 kwa mkoa wa Mtwara ulilenga kufikia
wanafunzi 10,200 wa shule za msingi kuwapatia elimu ya afya, namna ya
kujisitiri wakati wa hedhi na kupatiwa vifaa vya kujisitiri ambapo
katika thamini yake iliyotolewa chini ya utekelezaji wake kwa mkoa wa
Mtwara umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuweza kupunguza
tatizo la utoro.
“Lengo
la mradi ni kufikia wasichana 10,200 kwa mkoa wa Lindi na Mtwara lakini
kwa mkoa wa Mtwara wanafunzi wapatao 7,077 tayari wamefikiwa na
tumekuwa tukiwapatia elimu juu ya hedhi, elimu itakayomsaidia pindi
anapokuwa kwenye hedhi afanye kitu gani pamoja na elimu ya afya na
madhara ya mimba za utotoni sambamba na kumsaidia vifaa vya kujisitiri
(pedi) na hii ni kutokana na kuwa suala la hedhi halizungumziwi kabisa
katika jamii yetu hivyo mtoto anapata changamoto na kumpelekea kukosa
shule kati ya siku 2 hadi tano ndani ya mwezi mmoja na kumrudisha nyuma
kieleimu,”alisema Chalambo.
Aidha
alisema changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo ni
pamoja na baadhi ya shule kukosa miundombinu kama vyoo na chumba maalumu
kwaajili ya kusaidia wasichana katika masuala ya afya na kuwa, Mradi
huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili itakuwa mkoa wa
Lindi.
“Katika
kutekeleza mradi huu hatuwezi kufanikiwa bila ya miundombinu,
tumegundua shule nyingi vyoo sio vizuri, kwahiyo bila kuendana na
miundombinu sahihi hatuwezi kufanikiwa,”alisema Chalambo.
Akizungumza
kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Mtwara, Jose Kitenana alisema mradi
huo umeweza kuleta mabadiliko katika mkoa huo na kuwa serikali imekuwa
ikifanya kila jitihada kuhakikisha miundombinu ya shule inakuwa rafiki.
“Mpango
huu ni mzuri na kwa sisi serikali hatuwezi kufanya kila jambo, hivyo
kuna wadau tunashirikiana nao kama T-Marc kutoa elimu ya afya kwa
wanafunzi kwa udhamini wa Vodacom Foundation ili kusaidia watoto wetu wa
kike, na suala la miundombinu bado zipo taratibu ambazo zinafanyika
kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki,”alisema Kitenana
Naye
Mkuu wa Vodacom Foudation, Renatus Rwehikiza alisema wamekuwa wakitoa
misaada mbalimbali kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa
wanatekeleza mradi wa hakuna wasichoweza kwa lengo la kuongeza
mahudhurio ya watoto shuleni na kuwa itapunguza kasi ya magonjwa,utoro
na mimba za utotoni.
“Vodacom
Foundation inatoa misaada kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa
hivi tuna mradi wa ‘hakuna wasichoweza’ umegharimu kiasi cha 480
milioni ambao umetekelezwa kwa awamu na sasa kwa mkoa wa Mtwara
tumefikia ukingoni tunasubiri kupata tathmini ya huu mradi na awamu ya
pili tutakuwa mkoa wa Lindi lakini nina imani kwa kiasi kikubwa
utasaidia kupunguza ile kasi ya utoro na mimba za utotoni na kumwezesha
mototo wa kike kutimiza ndoto zake,”alisema Rwehikiza
Akizungumza
mwanafunzi, Doreen Mvungi alisema mradi huo umeweza kuwapa maarifa
namna ya kukabiliana na changamoto walizokuwa wakizipata pindi
wanapopatwa na hedhi shuleni na kuondokana na aibu ya kuzomewa
waliyokuwa wakiipata toka kwa wavulana.
“Najivunia
kuwa sehemu ya walionufaika na Mradi huu ni mkombozi umetupa elimu ya
afya, elimu namna ya kujisitiri tunapokuwa katika hedhi na imewasaidia
wengi kwani siku hizi hamna tena ile zomea zomea na hata mahudhurio ya
darasani yameanza kuwa mazuri kwa sisi wasichana tofauti na zamani
msichana alipokuwa akipatwa na ile hali anashindwa kujua nini cha
kufanya,”alisema Doreen.
Meneja
Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark Tanzania Doris
Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wa
elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao
ulikuwa unaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili
wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na
Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
Baadhi
ya wadau wa elimu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye warsha maalumu ya
mrejesho wa mradi wa”Hakuna wasichoweza” unaowapa elimu ya hedhi na
vifaa vya kustiri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao
mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na
T-Mark Tanzania.
No comments:
Post a Comment