RAIS DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WAMA SHARAF LINDI
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda baada ya kuwasili kwenye
eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi Mjini
kwenye sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bwana Ibrahim Sharaf, Rais wa Sharaf
Group of Companies ya nchini Dubai mara baada ya kuwasili kwenye Shule
ya Sekonadi ya Wasichana WAMA Sharaf huko Lindi. Rais Kikwete alikuwa
mgeni rasmi katika sherehe ya uzinduzi wa Shule hiyo.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiondoa kitambaa kwa kushirikiana na Bwana Ibrahim
Sharaf aliyefadhili ujenzi wa Shule ya Wasichana ya WAMA Sharaf ikiwa
ni ishara ya kuizindua rasmi. Baadaye Rais Dkt. Kikwete akishirikiana na
viongozi wengine walisaidia ujenzi wa shule hiyo kukata utepe ikiwa ni
mwendelezo wa sherehe za ufunguzi rasmi wa shule hiyo huko Lindi.
Rais DKT. Jakaya Kikwete akifuatana na Bwana Sharafuddin Sharaf na wageni wengine wakitembelea shule.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na wageni waalikwa wakiangalia wanafunzi wakifanya
majaribio mbalimbali ya masomo ya sayansi kwenye Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya WAMA Sharaf huko Lindi baada ya kufunguliwa rasmi.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma wakiwatembeza wageni waalikwa sehemu mbalimbali za shule hiyo.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akitoa tunzo maalum kwa Kampuni ya Sharaf Group ya
Dubai kwa msaada wao wa kujenga shule hiyo huko Lindi.
No comments:
Post a Comment