MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA SHULE YA SECONDARY J.K NYERERE HUKO TARIME
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Capt. Mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kwa ziara ya siku mbili mkoani humo tarehe 2.10.2015. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara.
Mama Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.
Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha Nyamwaga.
Mama Salma Kikwete baada ya kukata utepe hapa anakiondoa kitambaa kukamilisha sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo.
Mama Salma Kikwete akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Capt. Mstaafu Aseri Msangi na Ndugu Glorius Luoga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuondoa kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa uboreshaji wa hospitali hiyo.
Baada ya kuzindua rasmi uboreshaji wa hospitali ya Wilaya ya Tarime, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete anapanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo la hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu Glorius Luoga muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya uzinduzi wa Shule ya Sekondari J K Nyerere.
Mama Salma Kikwete akipiga picha na wanachuo wanaosomea uuguzi katika Hospitali ya Wilaya Tarime
No comments:
Post a Comment