KONGAMANO LA ELIMU YA JUU LAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA
Afisa
Masoko wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) wa Tawi la Arusha,
Regina Lema akitoa maelezo kwa mmoja ya wageni waliofika katika
maonyesho yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa
kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT)
yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu ya
juu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Baadhi ya wakuu wa vyuo na viongozi mbalimbali wa Taasisi zinazohusika na masuala ya elimu wakipata maelezo toka banda la GEL.
Mwanafunzi
wa Chuo cha St. Joseph akitoa maelezo jinsi mfumo wa Mita za kipekee
za kutoa umeme kufuatana na matumizi ya mteja ambapo hata kama wateja
wapo kumi kila mmoja anaweza tumia kutokana na mahitaji yake.
Chuo
Kikuu cha Muhimbili cha jijini Dar es Salaam kimeshiriki katika
maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa
kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT)
yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu
lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Mmoja
ya washiriki ambaye amebuni mtambo wa kuchuja maji, akitoa maelezo kwa
Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania aliyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini
(TCU), Profesa Yunus Mgaya akiwaonyesha ubora wa chujio linalotumika
kutoa maji safi na salama.
Maprofesa wakiwa katika kongamano la saba la elimu ya juu 2015 lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015 jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment