Tukielekea maadhimisho ya SikuYaMtoto wa Afrika, @SemaTanzania kupitia ElimikaWikiendi italeta mjadala wa Malezi
Friday, 10 June 2016
Wednesday, 8 June 2016
Wanafunzi wa darasa la Saba waaswa kuongeza bidii katika masomo ya Sayansi
Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.
Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha
Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.
Wito huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.
Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).
Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.
Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.
Tuesday, 7 June 2016
SSRA YATOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII KWA WAKULIMA, VYUO VYA UALIMU NA VETA KATIKA MIKOA YA RUKWA, KIGOMA NA KATAVI
Mgeni rasmi Kaimu RAS Mkoa wa Rukwa Bw. Abubakary Kunenge, akitoa hotuba wakati wa ufungizi wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wakulima wa MVIWATA Rukwa, Kulia ni Mwenyekiti wa MVIWATA Rukwa Bi. Lydia Ruhilo na kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Mohamed Nyasama.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kutoka SSRA wakati wa Semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Rukwa hivi karibuni.
Afisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Samuel Nzunda akiwasilisha mada wakati wa semina ya elimu ya Hiafadhi ya Jamii mkoani Rukwa.
Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa Chuo cha VETA-Kigoma mara baada ya semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii iliyoendeshwa na SSRA mkoani humo hivi karibuni.
Bi Carina Wangwe, kutoka SSRA akifafanua jambo wakati wa semina ya elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau mkoani Kigoma.
Wanafunzi wa Chuo cha UfundiStadi – VETA Kigoma wakisikiliza kwa makini mada kutoka kwa maofisa wa SSRA.
Sehemu ya wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoani Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka SSRA wakati wa semina za elimu kwa Umma mkoani humo.
Monday, 6 June 2016
MSANII DIAMOND ATOA MSAADA WA MADAWATI 600 KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. MAKONDA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akimpongeza Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na kutoa mchango wake wa madawati yapatayo 600 kwa ajili ya kuchangia maendelea ya mkoa. Akiongea katika makabidhiano hayo msanii huyo alisema ni jambo jema kwao kuweza kujitolea mchango huo ili kuweza kumuunga mkono Mhe. Makonda katika kukabilana na changamoto za elimu.
Mkurugenzi wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akiongea mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati yapatayo 600 kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaa.
Makonda akitoa shukrani zake za pekee kwa Mkurugenzi
wa WCB, msanii Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' kwa kuweza kutoa madawati 600
ikiwa ni mchango wake katika elimu ya kuweza kufanya wanafunzi kukaa sehemu
salama. Mhe. Makonda alisema kuwa wakati umefika kwa wasanii wakaweza kujitoa
katika jamii ambayo imekuwa ikiwapa wao sapoti na msanii Diamond amekuwa wa
kwanza
kuonyesha moyo wa pekee kwa kurudisha fadhila.
Makonda akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa WCB
mara baada ya kumtembelea ofisini kwake.
Mwanafunzi amtumia Obama kutatua shida ya maji nchini.
Juzi, Eva ambaye anasoma Shule ya Sekondari Mlowa mkoani
Iringa, alimkabidhi barua nyingine ya kampeni yake ya kupambana na uhaba wa
maji, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoianzisha kutokana na majibu
aliyoandikiwa na Rais Obama akieleza matatizo yaliyopo katika Jimbo la Isimani
mkoani humo.
Mwanafunzi wa kidato cha pili, Eva Shedrack (16) ameanzisha kampeni
ya kupambana na uhaba wa maji baada ya kupokea majibu ya barua yake
aliyoandikiwa na Rais Barack Obama wa Marekani.
Awali, Eva alimwandikia barua rais
huyo akieleza kuhusu uhaba wa maji nchini ambayo ilisomwa katika baraza
kuu la Umoja wa Mataifa (UN), Septemba mwaka jana.
Juzi, Eva ambaye anasoma Shule
ya Sekondari Mlowa mkoani Iringa, alimkabidhi barua nyingine ya kampeni yake ya
kupambana na uhaba wa maji, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoianzisha kutokana
na majibu aliyoandikiwa na Rais Obama akieleza matatizo yaliyopo katika Jimbo
la Isimani mkoani humo.
Katika barua yake kwa Waziri Mkuu,
Eva alisema ameanzisha kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la ‘Simama na Eva’
ambayo imejipanga kusaidia kutatua kero ya maji vijijini.
Sunday, 5 June 2016
WALIOTIMULIWA UDOM,WATOA YA MOYONI
Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa
Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.
Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.
“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.
“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.
“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”
Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.
Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.
“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.
Udom yazungumza
Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.
“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.
Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.
“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.
Subscribe to:
Posts (Atom)









