Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified" Mjema alizindua uwanja huo leo katika hafla fupi iliyofanyika katika
shule hiy.Kushoto ni Jokate akishuhudia tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye
hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala.Ndugu
Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate
Mwegelo.
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi
wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa
Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa
Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto)
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia kampeni yake
ya "Be Kidotified" uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa pili
kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa
na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos
Mgongolwa.
Kwa habari zaidi
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya "Be Kidotified". Alisema
kuwa amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya kuendeleza
michezo na taaluma.
Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni
yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja
utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli) kwa
Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.
Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule
hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali.
Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi milioni 50.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano
kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika
shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya
michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa
changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo
ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo vitamwezesha mshiriki
kupata ajira. Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma
maendeleo ya michezo nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha
wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo, lakini
alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje ya darasa ikiwa
pamoja na michezo na kujifunza mengi. “Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa
nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini
niliyotafuta kuhitimisha ujenzi wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi
wa shule ya Sekondari ya Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine,
”
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji
Foundation, na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya
‘Be Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule nyingine
za hapa jijini,” alisema Jokate. Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa
chama zinazoongoza hapa nchini katika mitindo, urembo na burudani kabla ya
kuamua kupanua wigo kwa upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na
kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti brand’ akiwa
na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli mbalimbali za
ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.
Habari kwa Hisani ya Michuzi