Monday, 6 June 2016

Mwanafunzi amtumia Obama kutatua shida ya maji nchini.

Juzi,  Eva ambaye anasoma Shule ya Sekondari Mlowa mkoani Iringa, alimkabidhi barua nyingine ya kampeni yake ya kupambana na uhaba wa maji, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoianzisha kutokana na majibu aliyoandikiwa na Rais Obama akieleza matatizo yaliyopo katika Jimbo la Isimani mkoani humo.
Mwanafunzi wa kidato cha pili, Eva Shedrack (16) ameanzisha kampeni ya kupambana na uhaba wa maji baada ya kupokea majibu ya barua yake aliyoandikiwa na Rais Barack Obama wa Marekani.
Awali, Eva alimwandikia barua rais huyo akieleza kuhusu uhaba wa maji nchini ambayo  ilisomwa katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UN), Septemba mwaka jana.
Juzi,  Eva ambaye anasoma Shule ya Sekondari Mlowa mkoani Iringa, alimkabidhi barua nyingine ya kampeni yake ya kupambana na uhaba wa maji, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoianzisha kutokana na majibu aliyoandikiwa na Rais Obama akieleza matatizo yaliyopo katika Jimbo la Isimani mkoani humo.
Katika barua yake kwa Waziri Mkuu, Eva alisema ameanzisha kampeni hiyo inayojulikana kwa jina la ‘Simama na Eva’ ambayo imejipanga  kusaidia kutatua kero ya maji vijijini.

No comments:

Post a Comment