Thursday, 16 June 2016
Sunday, 12 June 2016
WANAFUNZI WA KITIVO CHA SHERIA WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (MLIMANI) WAFANYA SHEREHE YA KUAGANA JIJINI DAR ES SALAAM.
Wanafunzi wanao soma sheria chuo kikuu cha Dar es salaam,wakiwa katika sherehe ya kuagana kabla ya kufanya mtihani wa mwisho,baada ya kusoma kozi hiyo kwa miaka mnne hapo chuoni.
Katika mapozi tofauti tofauti
Hii ni keki yenye nembo ya chuo kikuu cha dar Dar es salaam,kuashiria wanatambua umuhimu wa chuo chao.
picha ya makundi ya wanafunzi hao katika sherehe hiyo iliyo fanyika jijini Dar es salaam.
Wana sheria watarajiwa wakiwa katika ubora wao katika shughuli hiyo.
Huyu ndio Mtaalamu wa Sheria za Keki pale chuo kikuu cha Dar es salaam,katika ubora wake.
Friday, 10 June 2016
HELLEN, MTANZANIA ALIYETAJWA NA FORBES KUWA BILIONEA AJAE
Jina lake ni Hellen Dausen na umri wake ni miaka 29 ( November 1986) na aliipiga chini ndoto yake aliyokaa nayo miaka kumi bila kumfanikisha kisha akaingia kwenye mbio za Ubilionea na kitu kingine kabisa maishani mwake.
Unaambiwa Jarida la FORBES ambalo limekua na nguvu duniani na kutoa ripoti mbalimbali zikiwemo za uchumi na watu na utajiri wao, lilikua na list ya idadi ya vijana takribani elfu mbili lakini Hellen akaibuka miongoni mwa vijana 30 wa Afrika wenye fikra na mikakati ambayo ni utajiri wa siku chache zijazo.
Ishi ndoto zako kijana.
NAIBU WAZIRI WA MAZINGIRA NA MUUNGANO MGENI RASMI TAMASHA KUBWA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA MBEYA
Katika kutengeneza Msingi mzuri kwa wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya inafanya Maonyesho Makubwa ya Ajira na Ujasiriamali siku ya tarehe 11 June 2015.
Katika kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za ajira wamealikwa kutoa mada na kuonyesha uzoefu wao kwenye ujasiriamali na utendaji kazini. Watoa mada walioalikwa kwenye Tamasha Hilo ni; Imani Kajula ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba amba ye ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Wakili Alberto Msando – Wakili maarufu wakujitegemea na mjasiriamali, Victor Kikoti Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – MenejawaTawi la CRDB Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo ni Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mh.LuhagaMpina.
Upatikanaji wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu ya kutatua changamoto hiyo.
USIKOSE KESHO KWENYE ELIMIKAWIKIENDI KWENYE UKURASA WA TWITTER TUJUMUIKE WOTE KESHO.
Tukielekea maadhimisho ya SikuYaMtoto wa Afrika, @SemaTanzania kupitia ElimikaWikiendi italeta mjadala wa Malezi
Wednesday, 8 June 2016
Wanafunzi wa darasa la Saba waaswa kuongeza bidii katika masomo ya Sayansi
Mtaalam kutoka Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Pius Lugomela (mwenye shati la bluu), akitoa malezo kuhusu vifaa mbalimbali vya upimaji ramani vilivyoko kwenye maabara ya Skuli iyo.Vifaa kwenye maabara hiyo pia hutumika kwa ajili ya shuguli za ufundishaji, utafiti na ushauri wa kitaalamu kwenye maenneo ya upimaji ardhi na ramani.
Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mazingira (Environmental Engineering) Dr. Fredrick Salukele akiwaelezea wanafunzi matumizi ya vifaa mbalimbali vitumikavyo kwenye shughuli za ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri wa kitaalam, mfano wa vifaa hivyo ni Gaschromatograph kinachoonekana kwenye picha
Wanafunzi wakiangalia kwa makini baadhi ya kazi za ubunifu majengo zilizo fanywa na wanafunzi wa Skuli ya Ubunifu Majengo wa Chuo Kikuu Ardhi. Kubuni aina mbalimbali za majengo ni moja kati ya mahitaji kwenye mtaala wa kufundishia program ya Usanifu Majengo ya Chuo Kikuu Ardhi
Chuo Kikuu Ardhi kimetoa wito kwa wanafunzi wanaosoma darasa la saba kote nchini kufanya bidii katika masomo ya Sayansi na Hisabati ili waweze kujenga msingi imara na kuandaa mazingira ya kujiunga na fani za Sayansi katika elimu ya Sekondari na vyuo vikuu.
Wito huo huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na baadhi ya wataalamu wa Chuo hicho mara baada ya kuwapokea wanafuzi 84 wa Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maximilian waliotembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho kwa lengo la kujifunza majukumu ya chuo hicho na elimu inayotolewa.
Wakiwa chuoni hapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kuitembelea Skuli ya Sayansi ya Mazingira na Teknolojia (Environmental Science and Technology) Skuli ya Ubunifu Majengo (School of Architecture and Design) na Skuli ya Sayansi ya Jiomatiki na Tekinolojia (School of Geospatial Sciences and Technology).
Aidha, Wanafunzi hao walipata fursa ya kuuliza maswali mbali mbali kwa wataalamu.
Ziara hiyo imelenga kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi ili waweze kupata alama za juu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita na kisha kujiunga na Chuo kikuu Ardhi ili baadaye wawe wataalamu katika fani mbalimbali za Ardhi na Mazingira.
Subscribe to:
Posts (Atom)

















